MWILI WA MWALIMU ALIYEPOTEA KATIKA MAZINGIRA YA KUTATANISHA WAPATIKANA UKIWA KATIKA HALI MBAYA ZAIDI WILAYANI LUDEWA


         Hilo hapo juu ni shimo na ndani yake kuna mwili wa mwalimu huyo aliyeuawa kikatili
 


            Baadhi ya wataalam wakiwa tayari kuutoa mwili huo katika shimo walilofukia mwili huo,

    
Tunaomba radhi kwa picha hizi  Ni mwili wa aliyekuwa mwalimu mkuu wa shule ya msingi muholo wilayani ludewa mkoani Njombe aliyeuawa kikatili na kufukiwa chini ya ardhi,

Askari wa jeshi la polisi Ludewa wakiwa wameubeba mwili wa aliyekuwa mwalimu huyo,


Na Maiko Luoga Ludewa,    Hatimae mwili wa aliyekuwa mwalimu mkuu wa shule ya msingi Muholo Katika kijiji cha muholo kata ya Luana wilayani Ludewa katika Mkoa wa Njombe mwalimu Majutho Haule aliyepotea katika mazingira ya kutatanisha mwezi mei mwaka huu umepatikana hapo jana september 21 mwaka huu katika eneo la daraja mbili nje kidogo ya kijiji cha muholo na katika shamba la mwalimu mwenzake Vinsent Haule.


Mwili huo umepatikana kwa ushirikiano mkubwa uliofanywa na wananchi wa kijiji cha muholo na Askari wa jeshi la polisi wilayani Ludewa baada ya kufanya doria kali katika kijiji hicho na kufanya mahojiano na baadhi ya watuhumiwa waliokuwa wakizidi kuhojiwa na askari polisi wilayani Ludewa na kukuta mwili huo ukiwa umefukiwa chini ya Ardhi ukiwa umeharibika vibaya.

Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Ludewa ambae pia ni mkuu wa wilaya ya Ludewa katika mkoa wa njombe Mh, Anathory K Choya amelaani vikali tukio hilo la kinyama na kusema kuwa atashirikiana kikamilifu na askari wa jeshi la polisi Wilaya ya ludewa pamoja na wananchi wenye nia njema ili kuhakikisha wahusika wa tukio hilo wanapatikana na kutiwa katika vyombo vya dora ili sheria ichukue mkondo wake.

Marehemu alipotea katika mazingira ya kutatanisha mwezi mei mwaka huu akiwa na usafiri wake aina ya pikipiki ambayo bado haijaonekana hadi sasa na jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi zaidi juu ya tukio hilo ikiwemo ni pamoja na kuhakikisha pikipiki hiyo inapatikana mara moja mahali ilipo.

www.maikoluoga.blogsport.com Tumezungumza na wananchi wa kijiji cha muholo kata ya Luana wilayani ludewa ambao kwapamoja wameonesha kusikitishwa kwao juu ya tukio hilo huku wakiamini kuwa hakuna mwalimu yeyote ambae atakubali kufanya kazi katika kijji chao.

Walimu kote wilayani Ludewa mkoani njombe wamelaani vikali tukio hilo na kusema kuwa wataungana pamoja kuwafariji ndugu, jamaa na marafiki hasa katika kipindi hiki kigumu ili kuweza kukemea tukio hilo la kikatili dhidi ya walimu.

Mwishoooooo.


Chagua kiongozi bora ili kuleta mabadiliko
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment