DC LUDEWA AAGIZA KUKAMATWA KWA MGOMBEA KITI CHA UDIWANI KUPITIA CHADEMA KATA YA MLANGALI


        Mkuu wa wilaya ya Ludewa mkoani NJOMBE Mh, Anathory Choya akizungumza na mtandao huu,



 Polisi wilayani Ludewa wasema wamejipanga kikamilifu kukabiliana na uhalifu wilayani humo.


  Na Maiko Luoga Ludewa ,
 Mkuu wa wilaya ya  Ludewa mkoani njombe MH, Anatory Choya ameliagiza jeshi la polisi wilayani hapa kumkamata Mara moja Kwa lengo la kumhoji mgombea udiwani kata ya Mlangali kupitia chama cha demokrasia na maendeleo Chadema anaeungwa mkono na vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi Ukawa kata ya mlangali bw.Amosi Basil Mtweve Kwa tuhuma za kuwapiga makada wawili wa ccm kata ya mlangali ambao ni Nelson Kyando na Samwel Mtweve wakazi wa mlangali na kuwashambulia Kwa matusi.


Ametoa agizo hilo mapema hii leo september 22 mwaka huu katika Ofisi yake wakati akizungumza na viongozi wa chama cha mapinduzi ccm kata ya Mlangali pamoja na mgombea kiti cha udiwani kata ya Mlangali kupitia chama cha mapinduzi ccm Mh, Khamis Kayombo na kusema kuwa kitendo cha mgombea huyo wa udiwani kata ya mlangali kupitia Chama cha demokrasia na maendeleo chadema kupiga wafuasi wa ccm ni kosa kubwa kisheria.

Kwaupande wake Mkuu wa polisi wilaya ya Ludewa Ocd Emmanuel Gari ya Moshi ameahidi kumfikisha ktk mikono ya sheria mtuhumiwa huyo haraka iwezekanavyo Ili kuweza kukomesha vitendo na matukio ya uhalifu kwa wanasiasa kwa kipindi hiki cha kampeni za kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika October 25 mwaka huu na kuongeza kuwa mgombea huyo atakamatwa na kushtakiwa kama mtuhumiwa wa kawaida.

Wanachama hao wawili wa chama cha mapinduzi ccm kata ya mlangali waliopigwa na Bw, Amosi Mtweve ambae ni mgombea kiti cha udiwani kupitia chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema wamesema kuwa hivi karibuni walikuwa katika moja ya Maeneo ya starehe Maarufu kama Baar wakiendelea kustarehe wakaambiwa na mgombea huyo wanywe pombe alizo nunua yeye kwa shart la kumchagua nao wakagoma na kujikuta wanapata kipigo hicho kikali.




Chagua kiongozi bora ili kuleta mabadiliko
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment