Mfululizo
wa uhalifu dhidi ya makanisa mbalimbali bado unaendelea katika Mkoa wa
Kagera ambapo makanisa matatu yamevunjwa na samani zake kuchomwa moto
ndani ya siku moja likiwa ni tukio la pili kutokea katika kipindi cha
wiki mbili sasa.
Kamanda
wa Polisi wa Mkoa wa Kagera Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi
Augustino Ollomi amethibitisha kutokea kwa matukio hayo na kwamba jeshi
la Polisi bado linaendelea na upelelezi kuhakikisha linawatia mbaroni
wale wote wanaohusika na vitendo hivyo.
Makanisa
yaliyoguswa na uhalifu huo ni pamoja na Kanisa la Kilutheri la Katoro
na lile la kijiji cha Musira ,pamoja na kigango cha Katoliki cha
kijiji cha Kituntu katika tarafa ya Katoro.
Uhalifu
huo umefanyika kwa staili ya kuvunja milango na kuchoma samani za
ndani ,tofauti na uhalifu wa wiki iliyopita ambapo makanisa matatu ya
kipentekoste yalichomwa moto na kuteketea samani pamoja na majengo.
Kamanda
wa Polisi wa Mkoa wa Kagera SACP Augustino Ollomi licha ya kuthibitisha
kutokea kwa uhalifu huo,anaelezea mikakati inayowekwa na jeshi hilo
kuhakikisha uhalifu huo hautokei tena katika nyumba za ibada.
Aidha
Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Kagera ambaye pia
ni Mkuu wa Mkoa huo John Mongella,ametoa tamko mara baada ya kumalizika
kwa kikao cha kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa juu ya matukio hayo.
Chagua kiongozi bora ili kuleta mabadiliko
Blogger Comment
Facebook Comment