Mchezaji
Ramadhani Singano’Messi’ ambaye amekuwa akikaa benchi tangu asajiliwe
kwenye kikosi cha Azam FC, kesho anaweza akacheza kwa dakika zote 90
wakati Azam itakapokuwa ikimenyana na Coastal Union kwenye mchezo wa
ligi kuu Tanzania bara utakaochezwa kwenye uwanja wa Azam Complex,
Chamazi.
Mtandao huu umezungumza na kocha
mkuu wa kikosi cha ‘wanalambalamba’ Stewart Hall kutaka kujua ni kwanini
nyota huyo amekuwa akisugua benchi kwenye kikosi cha Azam tangu ajiunge
na mabingwa hao wa Kagame licha ya kuwa na uwezo mkubwa wa kusakata
kabumbu.
“Messi alichelewa kujiunga na
timu (Azam) na tayari tulikuwa tumeshaiandaa timu kwa mfumo wetu
kulingana na wachezaji tuliokuwanao ambao haukumpa nafasi yeye kwakuwa
wakati tunaanza yeye hakuwepo”, amefafanua Hall.
“Baada ya yeye (Messi) kuingia
kwenye kikosi cha Azam tukaanza kutafuta namna ya kumuingiza kwenye
mfumo mpya na kumpa majukumu mapya. Alipokuwa Simba alikuwa anacheza
kama winga lakini kwenye kikosi chetu, mabeki wa pepembeni ndio
wanacheza kama mawinga kwahiyo yeye akawa nje ya mfumo”.
“Tulianza kumpa majukumu ya
kucheza namba 10 nyuma ya washambuliaji wawili na tangu ameanza kuvaa
majukumu hayo amekuwa akifanya vizuri kwenye mazoezi na sasa tumeona ni
wakati muafaka wa yeye kucheza kwenye kikosi cha kwanza”.
“Kwa maana hiyo kwenye mchezo wa
kesho Messi ataanza kwenye kikosi cha kwanza kwenye mchezo dhidi ya
Coastal Union baada ya kufanya vizuri kwenye mazoezi”.
Chagua kiongozi bora ili kuleta mabadiliko
Blogger Comment
Facebook Comment