Na Gabriel Kilamlya Njombe
Kauli hiyo imetolewa na kaimu katibu tawala mkoa wa Njombe bwana Gidion
Mwinami kwa niaba ya mkuu wa Mkoa wakati wa warsha ya siku moja
inayolenga kutoa elimu kwa viongozi hao na wataalamu wa afya juu ya
kwenda kuwahamasisha wahudumu wa afya katika kukabiliana na magonjwa
hayo Kwa Kutumia Dawa Mpya ya Ziora.
Kupitia Warsha hiyo Mwinami amesema anategea viongozi hao watakwenda
kuwa mabalozi wazuri wa kufikisha elimu hiyo kwa wataalamu wengine wa
afya ambao wamekuwa wakitoa huduma za magonjwa hayo kwa watoto huku
akisema takwimu zinaonesha kuwa ugonjwa wa kuhara upo kwa asilimia 32.3
ikiwa Nimonia ni asilimia 16.3.
Kwa upande wake Dokta Rukia Ali toka wizara ya afya Amesema wamebaini
kuwepo kwa changamoto mbalimbali katika utoaji huduma ya afya kwa watoto
hao ikiwemo baadhi ya wahudumu kutokuwa na uelewa mpana namna ya
kuwahudumia watoto hao katika kukabiliana na magonjwa ya Kuhara na
Nimonia.
Wakizungumza katika samina hiyo washiriki hao ambao ni wafamasia, wakurugenzi wa
Halmashauri pamoja na makatibu tawala wa wilaya za Mkoa wa Njombe
wamesema kuwa pamoja na mipango mizuri inayopangwa na wizara ya afya
chini ya ufadhili wa UNICEF Lakini bado upatikanaji wa dawa za magonjwa
hayo umekuwa mgumu.
Jackson Saitabau ni Katibu Tawala Mkoa wa Njombe Ambaye Wakati Akifunga
Warsha Hiyo Amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri Kwenda Kuwasimamia
Watumishi Wao Katika Idara ya Afya Ili Waweze Kutoa Vyema Huduma ya Mama
na Mtoto Kwa Lengo la Kupunguza Vifo Vya Watoto Chini ya Miaka Mitano.
Ufinyu wa Bajeti,Elimu duni Kwa Wataalamu wa Afya Pamoja na Uhaba wa
Dawa Kutokana na Kucheleweshwa na MSD ni Miongoni Mwa Sababu Zilizotajwa
Kukwamisha Dhamira ya Kukabiliana na Nimonia na Kuhara Kwa Watoto
Waliochini ya Umri wa Miaka Mitano Jambo Linasababisha Kuwepo Kwa Vifo
Kwa Watoto Hao Kila Mwaka.
Chagua kiongozi bora ili kuleta mabadiliko