Katika hali isiyo ya kawaida,Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Dr. John Magufuli leo alijikuta katika wakati mgumu baada ya kukutana na zomea zomea ya kundi la vijana waliovamia msafara wake akiwa njianI kuelekea Mbarali na kuanza kuimba wakidai Lowassa ndo Rais wao
Pamoja
na kadhia hiyo,Magufuli alifanikiwa kufika Mbarali na kuhutubia
maelfu ya wananchi ambao amewaahidi kushughulikia migogoro yao
ya muda mrefu ambayo imekuwa kete ya kuombea kura kwa baadhi
ya wanasiasa wenye uchu wa madaraka.
Dr.
Magufuli leo pia amefanya mikutano kadhaa ya kampeni mkoani
Iringa ambako alilazimika kumalizia viporo hivyo vilivyokuwa
vimebaki mkoani humo.
Wananchi kwa maelfu wakimsikiliza Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia huko Makambako mkoani Iringa ambako alipita leo kumalizia viporo vya mkoa huo kwenye kampeni zake.

@mpekuzi
Blogger Comment
Facebook Comment