Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, jana aligeuka mbogo baada ya kuamua kuwataja hadharani watu wanaohujumu kampeni zake kwa kujifanya mchana wako pamoja na usiku wakigeukia upande wa upinzani.
Akiwahutubia
wananchi wa mkoani Shinyanga jana katika mkutano wake wa kampeni
uliofanyika katika Uwanja wa CCM Kambarage, Dk. Magufuli, alisema kuna
mamluki wanaokihujumu chama hicho katika kuelekea uchaguzi mkuu
unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, mwaka huu.
Dk.
Magufuli aliwataja hadharani baadhi ya makada hao ambao wamekuwa
wakiipigia kampeni CCM mchana na usiku wakiwapigia wapinzani.
“Kuna
baadhi ya wana-CCM wanatujuhumu sana, wengine nawajua hata majina yao
bahati nzuri huwa sisemi uongo bali ukweli, kuna huyu Gasper mchana tunakuwa naye CCM lakini usiku anaungana na wapinzani,” alisema.
Hata
hivyo, kauli hiyo ya Dk. Magufuli ilipokelewa kwa mshangao na baadhi
ya wananchi na wanachama waliokusanyika uwanjani hapo, kwa kuwa baadhi
ya makada hao walikuwa wameketi jukwaa kuu wakifuatila hotuba yake.
Mwandishi
wa habari hizi alimshuhudia meneja kampeni wa mgombea huyo, Abdallah
Bulembo, akimfuata Magufuli na kumnong’oneza ghafla Magufuli
alibadilisha na kudai msaliti ni Gasper Anthony wala si Gasper Kileo aliyetajwa awali.
Hata
hivyo, Magufuli baada ya kumaliza hotuba yake alimfuata kada huyo na
kumkumbatia huku akimtuliza na kuendelea na msafara wake.
Kada
huyo aliyetajwa kuwa msaliti anadaiwa awali kuwa mpambe wa mgombea wa
urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward
Lowassa, anayeungwa mkono na vyama vinavyunda Umoja wa Katiba (Ukawa).
Akizungumza
katika mkutano huo wa kampeni, Kileo alisema alimuunga mkono Lowassa
akiwa CCM, lakini kwa sasa anamuunga mkono mgombea urais wa chama hicho,
Dk. Magufuli na wala kwa kilichotokea hatarajii kukihama chama.
Akiwahutubia
mkoani Shinyanga, Magufuli amesema hashangai wananchi kuanza kumwita
rais kwasababu hata yeye anajua kuwa ndiye atakayeibuka na ushindi mnono
kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu.
Alisema wagombea wengine wa nafasi ya urais ni wasindikizaji tu kama walivyo wapambe wa kwenye harusi.
Mpekuzi blog
Chagua kiongozi bora ili kuleta mabadiliko
Blogger Comment
Facebook Comment