Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameonesha kuunga mkono mwenendo wa mgombea urais wa CCM wakati wa kampeni ya Uchaguzi mkuu inayoendelea nchini, Mheshimiwa John Pombe Joseph Magufuli.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu imebainisha kwamba kuna baadhi ya watu walimfuata
Rais Kikwete na kumuambia kuwa Magufuli anashutumu na kusahihisha Serikali yake na utendaji wake kwenye mikutano ya kampeni.
“Wamepata kuja watu kwangu wakaniambia kuwa Mgombea wetu wa CCM anashutumu uongozi wangu. Niliwaambia hivi analofanya Mgombea wetu ni jambo sahihi na barabara kabisa na lazima afanye hivyo.”Amesema Kikwete.
Rais Kikwete ameyasema hayo, Jumanne, Septemba 22, 2015 wakati alipozungumza na wafanyakazi wa taasisi nne za Marekani ambazo kwa namna moja ama nyingine zimefanya kazi na Serikali yake katika miaka 10 ya uongozi wake mjini Washington, D.C.
Aidha, Kikwete amesema kwamba nchi ya Tanzania inahitaji mawazo mapya na mwelekeo mpya ulio tofauti na uongozi wake. Amesema aliwaambia kuwa asiporuhusu jambo hilo kufanyika, nchi itabakia pale pale ambako ameifikisha yeye suala ambalo ni makosa makubwa kwa sababu nchi yetu lazima isonge mbele kwa mawazo mapya, kwa uongozi mpya na kwa staili mpya ya uongozi.
Katika hatua nyingine Rais Kikwete amesema kuwa anatamani muda uende kwa kasi zaidi ili aweze kukabidhi madaraka ya kuongoza Tanzania kwa Rais wa Tano, ili yeye apate muda wa kumpumzika baada ya kazi ngumu ya miaka 10 ambayo ameilezea kama mzigo mkubwa.
Chagua kiongozi bora ili kuleta mabadiliko
Blogger Comment
Facebook Comment