Dr. Slaa, familia yake watimkia Marekani


Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbroad Slaa.
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbroad Slaa.
Habari zilizotufikia hivii punde ni kwamba aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, Dk. Willibrod Slaa pamoja na familia yake  wamekwea pipa kuelekea nchini Marekani na familia yake.

Taarifa hiyo imebainisha kuwa Dk. Slaa amekwishandoka nchini kuelekea Marekani pamoja na familia yake tangu jana jioni.
Inadaiwa kuwa  akiwa nchini  Marekani Dr Slaa  atajiendeleza katika kozi fupi katika tasnia ya Sheria na Lugha.
Aidha,katika mahojiano yake  na kituo cha televisheni cha Azam, Dk. Slaa amesema nyumba yake itakuwa chini ya ulinzi wa Jeshi la Polisi  kutokana na vitisho ambavyo amekumbana navyo tangu alipoamua kuachia ngazi Chadema.
Dk. Slaa amesema licha ya kuwa nchini Marekani   ataendelea kufuatilia yanayojiri nchini huku  akiahidi   kurudi kupiga kura  tarehe 25 octoba 2015.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: