Binti wa miaka 19 matatani kwa Ugaidi


POLISI-PERANCIS
Msichana mmoja mwenye umri wa miaka 19 anashikiliwa na polisi nchini Hispania, kwa tuhuma za kuwapa mafunzo watu wanaotaka kujiunga na kundi la Dola la Kiislamu nchini Iraq na Syria.
Vyombo vya usalama vimesema vilianza kumchunguza mwanamke huyo, baada ya kukamata vifaa kutoka kwa Ayoub Moutchou, mtuhumiwa wa Dola la Kiislamu mwenye asili ya Morocco, aliyekimbia mwezi Julai na kukamatwa nchini Ujerumani mwezi uliopita.
Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Ndani iliyotolewa, imeeleza kuwa mwanamke huyo alikamatwa kwenye mji wa kaskazini mashariki wa Figueres, karibu na mpaka wa Ufaransa.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: