Askofu wa kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amejitokeza na kujibu tuhuma zote zilizotolewa dhidi yake ikiwemo kuitwa mshenga na Dk Wilbroad Slaa wakati akitangaza kujiuzulu wiki iliyopita
Akizungumza na Waandishi wa Habari pamoja na wananachi wengine walio hudhuria katika mkutano huo Gwajima amesema kuwa kujiuzulu kwa Dr Slaa Chadema sababu sio ujio wa Mwanasiasa Edward Lowassa aliyepewa ridhaa ya kugombea urais kupitia umoja huo.
Amesema chanzo ni mchumba wake Bi. Josephine Mushumbushi aliyepinga ujio wa Edward Lowassa kwa kuwa aliona kwamba jina la Dr.Slaa litaenguliwa katika kinyang’anyiro cha Urais na kupewa Edward Lowassa suala litakalopelekea yeye kuukosa ‘ufirst lady’ kwa kuwa amesha waahidi ndugu zake na marafiki zake kuwa atakuwa mke wa Rais ikiwa UKAWA itapewa ridhaa ya kuchaguliwa kuiongoza Tanzania kwa miaka mitano ijayo.
Hatua hiyo imepelekea Bi Josephine kumzuia Dr.Slaa kuhudhuria mikutano ya Chadema wakati wa mchakato wa kumpokea Mwanasiasa Edward Lowassa hali iliyopelekea pia Dr. Slaa kutupiwa mabegi yake nje na kulazimika kulala kwenye gari lake nje ya nyumba yake.
Akizungumzia kuhusu maaskofu kuhongwa na Mwanasiasa Edward Lowassa Gwajima amesema kwamba anachofanya Dr.Slaa ni kuwafanya maaskofu wasiheshimike mbele ya jamii kutokana na kuwahusisha katika kashifa wasiyohusiaka nayo.
Katika hatua nyingine Gwajima amesema anayo mambo mengine mazito ya Dr. Slaa ambayo akiyaweka wazi umma utashangaa hivyo kumtaka Dr. Slaa ajitokeze tena kumjibu ili yeye ajitokeze na kusema yote hadharani.
0 comments:
Post a Comment