Na Maiko Luoga Ludewa
Mahakama ya
wilaya ya Ludewa katika mkoa wa Njombe hii leo September 21 mwaka huu
imesikiliza kesi ya kujiandikisha mara mbili katika daftari la kudumu la
wapigakura katika mfumo wa BVR inayomkabili bw, Eletheo Izack Mtweve
[30] mkulima kabila mpangwa mkazi wa kijiji cha Lufumbu kata ya Mlangali
katika wilaya ya Ludewa ambaye alitenda kosa hilo April 03 mwaka huu
majira ya saa tano asubuhi katika kituo cha kujiandikisha wapigakura
Ofisi ya kijiji Lufumbu.
Akisoma shtaka linalomkabili mtuhumiwa huyo mbele ya Hakimu wa Mahakama ya wilaya ya Ludewa katika mkoa wa Njombe Mh, Mohamed Siliti mwendesha mashtaka Emmanuel Mtairuka alisema kuwa mnamo Tarehe 03/04 mwaka huu majira ya saa tano asubuhi mtuhumiwa alitenda kosa hilo la kujiandikisha marambili katika daftari la kudumu la mpigakura ambapo mtuhumiwa huyo alianza kujiandikisha katika kituo cha Ofisi ya kijiji Lufumbu na baadae kujulikana kuwa amerudia kujiandikisha katika kituo cha Shule ya msingi Lufumbu.
Kwa mujibu wa Shahidi Bw, Thadei Haule 55 ambaye pia ni afisa mtendaji wa kijiji cha Lufumbu kata ya Mlangali katika wilaya ya Ludewa mkoani njombe aliyefika mahakamani hapo na kutoa ushahidi wake mbele ya hakimu huyo wa wilaya alisema kuwa siku ya tukio yeye alikuwa katika harakati za kusimamia zoezi hilo na Ghafla alipigiwa simu na mmoja ya mawakala wa chama cha mapinduzi ccm na kuambiwa kuwa kunamtu amejiandikisha mara mbili na baada ya kufanya uchunguzi katika vituo vya uandikishaji maafisa wa uandikishaji wakabaini kuwa nikweli mtu huyo alijiandikisha mara mbili katika vituo tofauti.
Alisema kuwa walimuhoji mtuhumiwa huyo juu ya kosa hilo alilotenda lakini alikana kutenda kosa hilo ndipo walipoamua kumpekua katika mifuko yake na kumkuta akiwa na vitambulisho viwili vya kupigia kura ambapo kitambulisho cha kwanza kilisajiliwa kwa jina la Eletheo Izack Mtweve alicho jiandikisha katika kituo cha ofisi ya kijiji Lufumbu na kitambulisho cha pili kilisajiliwa kwa majina ya Eletheo Saimon Mtweve kituo cha Shule ya msingi Lufumbu ndipo mtuhumiwa huyo alipelekwa katika kituo cha polisi mlangali na kufunguliwa kesi hiyo kisha kupelekwa Lumande.
Baada ya Shahidi kukamilisha ushahidi wake Hakimu wa mahakama alimpa nafasi mtuhumiwa kujibu tuhuma hiyo kama ni kweli au laa ndipo mtuhumiwa huyo bila ya maelezo yoyote alisema Ushahidi uliotolewa mahakamani hapo ni wakweli Huku Akikiri kutenda kosa hilo kwa madai kuwa hakuwa na sababu maalumu ya kufanya hivyo huku akiiomba mahakama kumpa muda wa kutoa maelezo ya kutosha juu ya kosa hilo alilolitenda.
Hatahivyo kesi hiyo imeahirishwa kutokana na mtuhumiwa kuomba muda mwingine wa kujieleza zaidi juu ya kosa hilo linalo mkabili na Itasikilizwa tena October 05 mwaka huu na mtuhumiwa amepelekwa rumande kwakuwa kesi yake haina dhamana.

Chagua kiongozi bora ili kuleta mabadiliko
Blogger Comment
Facebook Comment