Siku moja baada ya taasisi ya Twaweza kutangaza ushindi mnono kwa mgombea Urais wa CCM,Dkt.John Pombe Magufuli dhidi ya Mgombea Urais wa Ukawa Edward Lowassa, Kada wa chama cha Mapinduzi Januari Makamba ametaja sababu tano za mgombea wa UKAWA kupata asimilia chache katika utafiti huo.
Akizungumza na Waandishi wa habari leo katika ofisi ndogo za CCM jijini Dar es salaam Makamba amesema kuwa CCM haikushangazwa na matokeo ya utafiti wa taasisi huru ya Twaweza yaliyotangazwa jana ambayo yanatoakana na sababu tano zifuatazo;
- Siku UKAWA walipomteua Ndugu Edward Lowassa kuwa mgombea wao ndio siku CCM ilipohakikishiwa ushindi katika uchaguzi wa mwaka huu. CCM hawakumteua kwasababu waliamini hakuna namna ambapo Watanzania wengi watamchagua.
- Katika uchaguzi wa mwaka huu CCM wanafanya utafiti wao wa ndani wa kisanyansi kila wiki kujua mwenendo na mwelekeo wa kampeni na maeneo yanayohitaji nguvu mahsusi. Tangu waanze utafiti wao mwishoni mwa mwezi Agosti, karibu kila wiki asilimia za ushindi wa CCM hazijawahi kushuka chini ya asilimia 60 na zimekuwa zinapanda.
- Kazi kubwa anayofanya mgombea wetu, Ndugu John Pombe Magufuli, na mgombea-mwenza, Ndugu Samia Suluhu Hassan, kuzunguka nchi nzima kwa barabara na kuongea moja kwa moja na wapiga kura inazaa matunda. Wanawafikia wapiga kura wengi, hasa wa vijijini, na wapiga kura hao wanawaelewa.
- Kampeni kubwa zinazofanywa na wagombea Ubunge na Udiwani wa CCM na makada na viongozi wa Chama katika ngazi zote nchi nzima kila siku kumuombea kura Magufuli nazo zinazaa matunda.
<a
href='https://mpakasi.com/ads/www/delivery/ck.php?n=a08724c9&cb=Math.random()'
target='_blank'><img
src='https://mpakasi.com/ads/www/delivery/avw.php?zoneid=19&source=https%3A%2F%2Fmpakasi.com&cb=Math.random()&n=a08724c9'
border='0' alt='' /></a>
5. CCM inaamini pia migogoro ndani ya UKAWA katika kipindi hiki cha
uchaguzi iliyopelekea mitafaruku katika kuachiana majimbo na, baadaye,
kutokana na uteuzi wa Mgombea Urais wa UKAWA, kupelekea kujiuzulu kwa
viongozi wa muda mrefu na maarufu wa UKAWA, Profesa Ibrahim Lipumba na
Dr. Wilbrod Slaa, na migongano ndani ya NCCR-Mageuzi, yote haya
yamepunguza imani ya wananchi kuhusu uwezo wa vyama hivi kushika dola.Katika hatua nyingine matokeo ya utafiti huu ni ishara kwamba Watanzania wamempokea na kumuelewa Ndugu Magufuli na wako tayari kumchagua katika uchaguzi mkuu utakaofanyika tarehe 25,oktoba.
Chagua kiongozi bora ili kuleta mabadiliko
Blogger Comment
Facebook Comment