Meneja wa zamani wa Manchester
United Sir Alex Ferguson alitaka mshahara wake uongezwe maradufu baada
ya mshahara wa Wayne Rooney kuongezwa pakubwa 2010.
Rooney alikuwa ametishia kuhama United lakini mwishowe akatia saini mkataba wa kulipwa ujira wa £250,000 kila wiki.“Niliwaambia sikudhani ilikuwa haki kwa Rooney kulipwa mshahara mara mbili ya mshahara wangu,” Ferguson amesema kwenye kitabu kipya.
“[mwenyekiti mwenza wa United] Joel Glazer alisema: ‘Nakubaliana nawe kabisa lakini tufanye nini?’ Ilikuwa rahisi. Tuliamua hakuna mchezaji anayefaa kulipwa mshahara mkubwa kunishinda.”
Kwenye kitabu chake kipya kuhusu usimamizi chenye jina Leading , Ferguson anasimulia kuhusu kipindi cha mpito alipoondoka Manchester United 2013 baada ya kuwa kwenye usukani miaka 26, akisema: “Tungeliisimamia vyema.”
Raia huyo wa Scotland, aliyeshinda mataji mawili ya Ligi ya Kilabu Bingwa Ulaya, mataji 13 ya Ligi ya Premier, vikombe vitano vya FA na vikombe vinne vya League, alirithiwa David Moyes, aliyefutwa miezi 10 baadaye.
Lakini mkufunzi huyo mwenye umri wa miaka 73 anasema alitaka pia kuzungumza na aliyekuwa kocha wa Barcelona ambaye sasa ananoa Bayern Munich Pep Guardiola kabla yake kumteua Moyes.
Chagua kiongozi bora ili kuleta mabadiliko
Blogger Comment
Facebook Comment