SECONDARY SCHOOL sehemu ya 3



















SECONDARY SCHOOL

Sehemu Ya 3

Mtunzi..... MoonBoy

Simu No. +255714419487 WhatsApp

Ilipoishia Jana →↓↓

"heeeeeeee sasa utapanda wapi hapa na unaona hakuna kiti cha nyuma?"
"mi staki bwana nitakaa hata hapo mbele tu"
"jamani aisha mwenzio nina udhu wa kuswalia bwana"
"jamani sheby kwani ntakugusa???"
"hapana bwana we kama una nia ya kumuomba mungu utakuja ila kama huna basi"
"ila sheby?? ngoja basi nikuambie mwenzioo"
"uniambie nini?"
"kwani sheby.......

SONGA NAYO



Nilikua namsikiliza huku nikiwa nimekaa mbali kweli
"ila sheby?? ngoja basi nikuambie mwenzioo"
"uniambie nini?"
"kwani sheby utarudi saa ngapi?"
"mmmhhh nitarudi kama muda wa saa 3 hivi kwani lazima nipitie msaafu kidogo"
"msaafu?? msaafu ndio nini?"
"umeona sasa ee? kumbe hata vitabu vya mungu tu huvijui"
"mmhh poa basi nitakusubiria muda huo au vp?"
"sawa pia"

Basi Nikaendelea zangu na safari ya kwenda masjidi kumuomba mungu wangu.... Niliingia zangu msikitini na kua kulipia swala zangu ambazo zilinipita toka mchana....

Ilinichukua kama dakika 15 hivi hadi kumaliza. hivyo nikatafuta mahali nikae kwa kusoma vitabu vya mungu, kwa kuisubiria swala ya isha, Kwani saa hio ilikua ni mida ya saa 1:35 jioni, Baada ya muda huo kuisha niliswali swala ya isha mida ya saa mbili... baada ya kumaliza kuswali tulianza kusoma dua mbili tatu za kumuomba mungu kwa kila jambo. Nilikua ni mtoto wa kitajiri wa kwanza kwenda msikitini kumuomba mungu.... maana asilimia nyingi ya watoto wa kitajiri hua hawanaga muda wa kwenda katika nyumba za ibada. kwani wanaona tabu kuinama inama au kufumba macho na kupiga makofi kule kanisani. Ila mimi niliushangaza mtaa pamoja hata na msikiti kwa kuwa mtoto wa kitajiri ninaependa kumuomba mungu.. Hata mashehe walikua wakinipenda sana kutokana na heshma na malezi mazuri ambayo nililelewa na MWAJU

Basi tulimaliza kupiga dua pale msikitini tena mimi ndio nilikua naisoma hio du. Nilikua napenda sana kua ostadhi mzuri na mpaka nifikie kuwa shekhe.

Kama kawaida yetu waislamu tukitoka lazima tupeane mikono ili kuombeana kheri na kuagana kwa amani... zoezi hilo lilipoisha nilitoka zangu na kuchukua BMX yangu ( baiskeli ndogo za kisharo ) Niliondoka zangu na kuelekea nyumbani huku nikiimba zangu nyimbo za kaswida..... sasa nilipofika chocho moja hivi nilikutana na wahuni ambao ni vibaka wa mtaani. Duuuuuu nikajua leo naoshewa hapa heeeee..... ila uzuri na mimi pia sio haba katika swala la kujitetea....
"oyaaa vunga kwanza basiii"
Mmija wao alinisimamisha kwa ubabe kisha wakaja wote afu mmoja akawasha tochi na kunimulika usoni. huku wakiandaa visu na marungu
"aaaaa kumbe ni huyu chaliii? Asee tumteme ariif uyu si chalii yetu wa kitaa pale mjengoni"
"yupi uyo?"
"si sheby uyu asee"
"aaaaa Ah sheby? sole bhana chalii yetu hatujakujua bhana... tulijua ni ngararu flani kumbe wewe?"
"afu hainaga kwere kama utatuchomesha mafegi arifu ama nini chalii yangu?"
Nilijisachi fresh nikawatoa na buku 5. kisha wakaniachia nisepe zangu.

Hawa wahuni hata sikua nawajua kabisa ila wao wanasema wananijua kabisa ila mimi simfahamu hata ntu mmoja kati yao, Basi niliondoka zangu huku nikiwa naendelea kuimba nyimbo zangu za kaswida.

Sasa nilipofika mahali nilikumbuka kua aisha atakua ananisubiri, hivyo nilibadili njia nyingine ili nisikutane nae. maana hana jipya la kuongea

Nilifika nyumbani salama kisha nikaweka bmx yangu vizuri kabisa maana ndio usafiri wangu wa shule kama school bus litaniacha, Nilimkuta mama angu akiwa anacheki tv pamoja na mwaju

ukiona hili neno MWAJU basi ujue ni huyu mama alienilea mimi na zaituni yaani mfanyakazi wetu wa kwanza. Kwani anaitwa MWAJABU hivyo namkatishia na kumuita MWAJU.... ila mimi hua namuitaga ANTI kwani sihitaji kumuita jina lake hivyo ukisikia neno MWAJU basi ujue ni yeye... na ukisikia neno ANTI pia ni yeye huyo mwajabu ambae ni mfanyakazi wetu wa kwanza na ana umri mkubwa tu. kwani ametulea sisi watoto wote wa humu ndani.

Niliingia ndani na wafanya kazi kama kawaida yao ya kuongea sana si unajua tena utajiri nao safi afu saa zingine ni kero.
"mambo?"
"poa. ila siku zingine nisalimie salamu ya kiislamu sawa dadaa ee?"
"sawa"
Nilinyooka zangu mpaka juu, kwani gheto yangu ipo rosheni ya juu. Nilienda mpaka huko kisha nikaenda kuoga zangu.... si unajua vyumba vya kitajiri ni kila kitu humo humo.. bafu huko huko choo huko huko yaani kila taka taka huko ipo... TV ninayo tena ni ya ukutani yenye ukubwa wa inchi 40 kitu cha flati..

Swaga za mavazi ninayovaa ni swaga hizi hizi za kisasa. ila sivai mlegezo Nilitoka zangu kuoga kisha nikapaka mifuta yangu Afu nikashuka ili nikajumuike na wenzangu kule sebuleni. Nilipofika nilimkuta dada nusura anaangalia kipindi flani hivi cha BBA ( Big Brother Africa ) hua anakipenda sana
"shkamoo dada"
"marahaba mambo vp?"
"poa tu"
Dada yangu nusura hua sio mkubwa kiviile kwani ana umri wa miaka 24 na mimi nina 20 hivyo nilimuamkia kwakua ni dada yangu na kanipita kiumri. Hivyo hata yeye hua hapendagi nimuamkie. kifupi hapendi kusalimiwa. ila mimi ananiacha tu nimsalimie kwakua tunaheshimiana sana. Mara mama alikuja
"sheby ulienda wapi?"
"nilienda msikitini mam"
"ok na zaituni yuko wapi?"
"mmhh atakua yupo chumbani kwake labda"
"hebu kamuite"

Zaituni yeye pia yupo chumba cha juu, Yaani gholofani huko nilipo mimi na pia dada nusura pia yupo rosheni ya juuu.. kifupi ni familia yote tupo gholofani, na huku chini ni vyumba vya wafanyakazi wote kasoro mlinzi ndio hua haingiagi ndani kulala. kwani yeye ana kigeto chake pale pembeni ya geti...
Basi niliingia ndani kwa dada yangu huku nikiwa na furaha yangu binafsi.
"we?"
"we ndio nani?"
"unaitwa bwana maswali mengi ya nini?"
Nilikua naongea na zaituni. kwani hua haziivi kabisa mi na yeye kwani leo tupo sawa kesho tumekwaruzana. si unajya watoto wa kitajiri wanavyokua na masifa...
"unaitwa na mamaa"
"sasa si ninakuja"
"mama anakuita kwa haraka zai"
"mmhhh nipishe uko"
Alitoka na kuelekea huko chini kwa mama,
Nami nikawa nafata nyuma kwa kurudi sebuleni

"tayari ushamsikiliza?"
"ndio"
"sasa mbona umenuna?"
"nani kanuna?"
"mmhh haya"
"afu sheby njoo huku chumbani nikuambie"
"uniambie nini?"
"we si uje tu"
Niliingia chumbani kwake na kukaa kitandani. kwani kawaida ya watoto wa kitajiri huwa hawanaga masharti ya kuingilia katika vyumba vya webzie. tofauti na watoto wa kimasikini Kwani hua watoto wa kitajiri wanapokua wadogo walikua wakilala pamoja na ni jinsia tofaut kabisa ila wanalala kitanda kimoja... ila tusiende mbali sana kwani hata sisi wenyewe ndio jinsi ilivyo yaani mfano dada yangu zaituni anaweza akaja chumbani kwangu na kuanza kuangalia tv mpaka akasinzia kwenye kochi. kisha mimi nambeba na kumlaza hapo hapo kitandani kwangu. na sio kua ni kipindi hicho lahasha bali hata sasa hivi pia na ukubwa wake likija chumbani kwangu linasinzia na kulala kabisa.. na hata wazazi wakituona hawana la kusema kwani si ndugu?? na pia wazazi mfano mama anaweza akaja chumbani kwangu na akamkuta zai kalala chumbani kwangu. lakini kikubwa atakachoongea ni hivi
"mfunike dada yako brangeti"
Hivyo hata sasa hivi nikiingia katika chumba cha dada yangu hakuna mtu atakaesema lolote. tofauti na masikini

Maana najua familia ya kimasikini mtoto wa kiume akishafikisha umri wa miaka 15 haruhusiwi kuingia chumbani kwa mama yake au dada yake. na hio siku akiingia heeeeeeee atakula kibano kutoka kwa dingi duuu...

Na humu ndani aliokua akiizuia hii tabia ni Anti mwaju yeye hakua akiipenda hii tabia ya kulala wote chumba kimoja pindi mmoja wetu anaposinzia chumbani kwa mwenzake.... kwani hata mimi siku moja nilienda chumbani kwa zaituni ili anielekeze baadhi ya maswali niliopewa shuleni, kwani yeye yupo kidato cha 4 na mimi nipo kidato cha 3 hivyo nilienda chumbani kwake ili anikokotolee swali moja hivi la math ( hesabu ) sasa katika hali ya kuelekezana mimi nilijikuta nimesinzia na kulala hapo hapo chumbani kwake... na nilipozinduka usiku nilijikuta nimefunikwa vizuri tu tena nimelazwa vizuri sana, kuliko nilivyolala mwanzo... na nikiangalia pembeni naona zaituni anakoroma tu. Nilipomuuliza kesho yake kua nani alinilaza vizuri na kunifunika shuka? akanijibu kua ni yeye... hivyo tukawa tumeshazoana kila mmoja kulala kwa mwenzie. na hii tabia ipo mpaka leo na familia yetu pia imezoea kwani licha ya kulala kwa zaituni pia nilishawahi kulala kwa dada nusura. tena na ukubwa huu huu na ilikua hivyo hivyo kulazana vizuri na kufunikana mashuka... ila dada nusura hajawahi kuja kulala kwangu.. kwani yeye ndio dada yetu mkubwa hivyo mimi na zaituni ni watoto tunaefatana hivyo mazoea bado yapo kati yetu....... siku moja zaituni alilala chumbani kwangu na anti mwaju alikemea lile jambo lakini mama angu alikuja juu na kumuambia kua
"waache watoto wangu bwana kwani wakilala pamoja ni ishara ya upondo kwao kua wanakumbukia utoto. waache watoto walale"
Afu baada ya kusema hivyo mimi nilikua zangu naangalia kipindi cha kiislamu kwenye tv hivyo mama akaniambia kua
"sheby?"
"naam mama?"
"usimsumbue dada yako mwache alale tu"
Hivyo mpaka leo hii mmoja wetu akilala kwa mwenzie hali ni hio hio ya kufunikana na kulazana vizuri....

HIO ↑↑ ILIKUA NI HISTORIA FUPI YA MAISHA TULIOLELEWA NA WAZAZI WETU.... SASA TUENDELEE NA PALE ALIPONIITA CHUMBANI KWAKE

"fanya fasta mi nataka nikaangalie kaswida"
"mmhhh we nawe unapenda hizo nyimbo zako mbayaaaa"
"afu zai kejeli hua spendi"
"ok yaishe Sasa kuna kitu nataka nikuambie"
"kitu gani hicho?"
"ah ah we kubali kwanza"
"kwani ni kizuri?"
"ndio.. tena ni kizuri saanaaa"
"haya nimekubali"
"sogea sasa nikunong'oneze"
"mbona una masharti hivyo?"
"bwanaaaa sheby we si uje tu"
"haya niambie"
Nikamtegea sikio ili aseme hicho kitu anachotaka kusema
"mwenzio mimi nime.........
Chagua kiongozi bora ili kuleta mabadiliko
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment