Barcelona wapigwa 4-1 na Celta Vigo




Mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi mara baada ya mchezo kumalizika
Mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi mara baada ya mchezo kumalizika
Barcelona walipokezwa kichapo chao kikubwa zaidi La Liga wakiwa chini ya Luis Enrique baada ya kulazwa 4-1 na Celta Vigo Jumatano.
Kushindwa huko kulifikisha kikomo mapema rekodi yao ya kushinda mechi zao zote msimu huu.

Mshambuliaji wa zamani wa Liverpool Iago Aspas alifunga mawili baada ya Nolito kuanza ufungaji mabao dhidi ya klabu hiyo yake ya zamani.
Neymar alikomboa moja upande wa Barca zikiwa zimesalia dakika 10 mchezo kuisha, kabla ya nyota wa zamani wa Manchester City na Stoke John Guidetti kufungia wenyeji bao la nne.
Barcelona walikuwa wamepoteza mechi moja pekee kati ya 25 walizocheza majuzi zaidi La Liga.
Ushindi wa Celta uliwaweka kileleni mwa ligi kwa muda, lakini Real Madrid waliwabandua baadaye baada ya kulaza Athletic Bilbao.
Mkufunzi mkuu wa Barca Luis Enrique, alisema: “Kilichoamua mechi hii ni jinsi Celta walivyocheza. Walicheza vyema sana.
“Tulijaribu kuwatatiza lakini walituzidi ujanja. Timu inapokuwa bora kukushinda, huwa huna mengi ya kusema.
“Heri nishindwe na timu inayocheza kama Celta walivyocheza leo, bila kutumia hila, kushinda kwa kucheza vyema soka. Nawapongeza na natumai waendelee kucheza vivyo hivyo.”
Hiyo ilikuwa mara ya tatu kwa Barca kufungwa magoli manne katika mechi tisa walizocheza msimu huu.
Walilazwa 4-0 na Athletic Bilbao katika Super Cup ya Uhispania na pia walicharaza Sevilla 5-4 katika Super Cup ya Uefa
Chagua kiongozi bora ili kuleta mabadiliko
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment