>AGOMA KUONGELEA KIFUNGO CHA COSTA AKIOGOPA KUFUNGIWA YEYE!
FA, Chama cha Soka cha England, kimeweka msingi hatari kwa kuifuta Kadi Nyekundu ya Beki wa Arsenal Gabriel kwa mujibu wa Meneja wa Chelsea Jose Mourinho.Gabriel Paulista alipewa Kadi Nyekundu na Refa Mike Dean baad ya kumpiga Teke Diego Costa wakati wa Mechi ya Ligi Kuu England Jumamosi iliyopita ambayo Chelsea iliifunga Arsenal 2-0.
Jumatatu, Jopo la FA liliamua kuifuta Kadi Nyekundu ya Gabriel baada ya Rufaa na pia kumfungia Straika wa Chelsea Diego Costa Mechi 3 kwa kitendo chake cha kumpiga Beki wa Arsenal Laurent Koscielny bila Refa Mike Dean kuona tukio hilo.
Kufarakana kwa Costa na Koscielny ndiko kulizua mzozo kati ya Costa na Gabriel na Beki huyo kutolewa nje.
Baada ya uamuzi wa FA kufuta Kadi ya Gabriel na kumfungia Costa, Jose Mourinho amesema: “Sasa tunajua kisasi kinaruhusiwa. Hamna tatizo, unaweza ukalipiza!”
Hata hivyo Mourinho amekataa kuongea lolote kuhusu kufungiwa kwa Costa akidai anaogopa nay eye kufungiwa pia.
Nae Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, amesema: “Hii inaonyesha walivyoamua baada ya Mechi kitu ambacho kilipaswa kuamuliwa wakati wa Mechi!”
Wenger aliongeza: “Wameripea Asilimia 5 ya uharibifu uliofanywa dhidi yetu. Badala ya sisi kucheza 11 dhidi ya 10, tulicheza 10 dhidi ya 11!
Chagua kiongozi bora ili kuleta mabadiliko
Blogger Comment
Facebook Comment