David De Gea alirejeshwa Kikosi cha Kwanza cha Man United Mwezi huu baada ya kutupwa nje kutokana na sakata lake la kuhamia Real Madrid.
Jana, baada ya Kepteni Wayne Rooney kutoka Uwanjani alipobadilishwa na Memphis Depay katika Dakika ya 81, utepe wa Kepteni ulipelekwa kwa David De Gea.
Ingawa De Gea alikuwa Kepteni kwa Dakika 10 tu, uamuzi huo wa kumpa utepe ulimfurahisha mno Kipa huyo ambae alitoa posti kwenye Mtandao wake wa Twitter na kusema: “Ushindi mkubwa Jana! Sasa tufikirie wapinzani wetu wanaokuja na tuwe bora zaidi. Nasikia fahari kuvaa utepe wa Kepteni!”
Kitendo hiki cha De Gea kinaonyesha ni jinsi mambo yalivyobadilika kutoka lile sakata lake la kugomea Mkataba mpya na kisha kubakia kidogo tu ajiunge na Real Madrid lakini hilo kushindikana Dakika ya mwisho Uhamisho huo ulipochelewa kukamilika Siku ya Mwisho ya Dirisha la Uhamisho.
Huku ikitegemewa De Gea atabakia Man United kwa Miezi 10 tu hadi Mkataba wake na Man United kwisha na kuhamia Real bure, mambo yakabadilika na Kipa huyo kusaini Mkataba mpya wa Miaka Minne na Man United.
SOKA IN TANZANIA
Chagua kiongozi bora ili kuleta mabadiliko
Blogger Comment
Facebook Comment