MGOMBEA KITI CHA UDIWANI KATA YA MLANGALI KUPITIA CHADEMA AFUNGULIWA KESI KITUO CHA POLISI


Hawa ni vijana wa ccm Waliopigwa mlangali ambao ni bw, Nelson Kyando wa kwanza kutoka kushoto na bw, Samweli mtweve kulia,


 Nelson Kyando akionesha baadhi ya majeraha katika mwili wake aliyoyapata kwa kipigo cha mgombea wa Udiwani kupitia Chadema kata ya mlangali wilayani Ludewa,


                           Huu ni mguu ambao kijana wa CCM amepata jeraha


Samweli mtweve akiwa amevaa Tishirt ya ccm ambayo imelowa damu kutokana na kipigo,

Mgombea Kiti cha Udiwani kata ya Mlangali Kupitia chama cha mapinduzi CCM mh, Khamis Kayombo akizungumza na mtandao huu juu ya kupigwa kwa vijana wake wa wili wa chama cha mapinduzi CCM kata ya Mlangali ktk wilaya ya Ludewa.


Na Maiko luoga Ludewa

Mgombea kiti cha udiwani kupitia chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema anaeungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa katiba ya wananchi UKAWA katika kata ya mlangali wilayani ludewa katika mkoa wa NJombe Aliyefahamika kwa jina moja La Amosi akiwa na wapambe wake amejikuta akijiingiza katika kibano kikali kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu mwezi october mwaka huu mara baada ya kuwashambulia kwa kipigo makada wawili wa CHAMA CHA MAPINDUZI CCM katika kata hiyo ya mlangali.


Mgombea kiti cha udiwani kupitia chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema anae ungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa katiba ya wananchi UKAWA katika kata ya mlangali wilayani ludewa katika mkoa wa NJombe Aliyefahamika kwa jina moja lA Amosi akiwa na wapambe wake amejikuta akijiingiza katika kibano kikali kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu mwezi october mwaka huu mara baada ya kuwashambulia kwa kipigo makada wawili wa CHAMA CHA MAPINDUZI CCM katika kata hiyo ya mlangali.


Makada hao wawili wa chama cha mapinduzi ccm kata ya mlangali ambao wameshambuliwa kwa kipigo kikali nipamoja na Bw, Nelson Kyando na Samweli Mtweve wote ni wakazi wa kijiji na kata ya mlangali wilayani Ludewa ambapo imedaiwa kuwa tukio hilo limetokea September 19 mwaka huu majira ya saa mbili usiku katika baa ya mfanyabiashara mmoja aliyefahamika kwa jina la Kayombo.

Mgombea huyo wa Chadema pamoja na Wapambe wake wengi wakiwa katika baa hiyo tena wakiwa wamelewa waliwapa kipigo kikali vijana hao ambao ni wanachama wa CCM kwa madai kuwa walikataa kunywa pombe za mgombea huyo kwakuwa mgombea huyo wa chadema alisema kuwa kila anaekunywa pombe alizotoa yeye kama mgombea udiwani kupitia chadema basi akubali kukipigia kura chama cha Chadema hasa katika nafasi hiyo ya Udiwani.

Wakizungumza na www.maikoluoga.blogsport.com wakiwa maeneo ya mlangali ndani majeruhi hao wamesema kuwa september 19 mwaka huu majira ya saa mbili usiku walifika katika baa hiyo ya Bw, Kayombo na kumkuta mgombea huyo wa udiwani kata ya mlangali akiwa na wapambe wake wakiwa wanakunywa pombe aina ya Bia na kuwalazimisha makada hao wa ccm kunywa pombe hizo kwa makubaliano ya kumpigia kura kupitia chadema na ndipo makada hao wa ccm wakagoma kutumia vinywaji hivyo vilivyokuwa na mashert makali na kujikuta wakiangukia kwenye kipigo kikali na kuumizwa vibaya hasa katika paji zao za uso, miguuni na mikono yao kuteguka.

Bw, Nelsoni Kyando ambae ni miongoni mwa walio pata kipigo hicho amesema kuwa ameumizwa vibaya katika mguu wake wa kulia pamoja na maeneo ya kifuani na kujikuta akikaa muda mrefu bila kuwa na fahamu huku akiiomba mamlaka husika hasa jeshi la polisi kutolifumbia macho jambo hilo kwakuwa ni kitendo cha kikatili na ubabe ambao hauna faida kwa wagombea hasa kwa kipindi hiki cha kampeni kuelekea uchaguzi mkuu na wakati huohuo bw, Samweli mtweve alidai kuwa alivalia shati la chama cha mapinduzi CCM Na baada ya kuweka wazi kugoma kunywa bia hizo zilizoandaliwa na mgombea wa chadema naye akajikuta akikabwa loba kali na mgombea huyo wa chadema na kula kipigo kikali pamoja na kutokwa damu puani mdomoni na Uso ukipata majeraha na kushindwa kuona kikamilifu.

Khamisi Kayombo ni mgombea Kiti cha udiwani kata ya Mlangali katika wilaya ya Ludewa na mkoa wa Njombe Kupitia chama cha mapinduzi CCM amelaani vikali kitendo cha mgombea huyo wa CHADEMA Kuwavamia na kuwapa kipigo vijana hao wawili wa chama cha mapinduzi na kusema kuwa amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa hizo na kusema kuwa wagombea wote wa Udiwani , Ubunge, Pamoja na Kiti cha Uras, Wa jamuhuri ya muungan wa Tanzania ni bora wakawa watulivu hasa kwa kipindi hiki cha uchaguzi mkuu ili wananchi waweze kuwachagua viongozi bora wa kuwaongoza kwa kipindi chote cha miaka mitano ijayo. 

Kwa upande wake mkuu wa kituo cha polisi mlangali amekili kutpokea tukio hilo na kufungua kesi ya jinai dhidi ya mgombea huyo huku akisema kuwa taarifa zaidi zitaendelea kutolewa juu ya tukio hilo huku akiiasa jami kuwa na utulivu hasa kwa kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu.

Chagua kiongozi bora ili kuleta mabadiliko
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment