WIKI YA NENDA KWA USALAMA BARABARANI NJOMBE KUANZA AGOSTI 27 HADI SEPTEMBA 2,2015
Kamanda wa Polisi Kikosi Cha Usalama Barabarani Kelvin Ndimbo Akizungumza na mtandao huu juu ya kusogezwa mbele kwa maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani yaliyotakiwa kuzinduliwa agosti 22 mwaka huu mkoani Njombe na badala yake agosti 27.
Mmiliki wa Mtandao huu Bwana Gabriel Kilamlya Akihojiana na Baadhi ya Madereva Katika Kituo Kikuu Cha Mabasi Mjini Njombe juu ya Kutarajiwa kuzinduliwa kwa wiki ya nenda kwa usalama barabarani mkoa wa Njombe Hapo Agosti 27 Mwaka Huu.
Hapa ni Katika Kituo Kikuu Cha Mabasi Mjini Njombe
Huyu ni Ajenti wa Usafirishaji Katika Mabasi ya Kampuni ya OTA HIGH CLASS Mjini
Habari na Barnabas Njenjema NJOMBE
Wakati Jeshi la Polisi Mkoani Njombe Kikosi Cha Usalama Barabarani likitarajia kuzindua wiki ya nenda kwa usalama barabarani Leo agosti 27 mwaka huu baada ya kuahirishwa agosti 22 Baadhi ya Madereva wa mabasi ya abiria wamesema tochi za kisasa zinazotumika na askari Zinapaswa Kutumiwa kadri ya malengo yaliyokusudiwa.
Hapa ni Kituo Kikuu Cha Mabasi Mjini Njombe Ambako mtandao huu Umezulu Ili Kujifunza namna Madereva Hawa Wanavyoipokea Wiki ya Nenda Kwa Usalama Barabarani Ikiwa Hali niliyoikutana nayo Juu ya Tochi za Kisasa Zinazofahamika Kwa Jina la Speed Rader ni Lawama.
Lakini Wengine Wameonekana Kupongeza Hatua ya Serikali Kuleta Tochi Hizo Ambazo Zinadaiwa Kufanya Kazi Kikamilifu Pasipo Kuacha Chembe ya Shaka Kwa Magari Yanayokamatwa.
Wakizungumza na www.gabrielkilamlya.blogspot.com baada ya kutembelewa na kituo hiki kuoana namna madereva hao wanavyoyapokea maadhimisho hayo wamesema kuwa tochi hizo zimekuwa zikitumika hata kwenye maeneo ambayo sio rasmi.
Wamesema Tochi hizo huenda zikawa kwa ajili ya kuwanufaisha baadhi ya askari kwani baadhi yao wanadaiwa kujificha na
pindi gari inapotokea ndipo wao kuibuka barabarani.
Kwa upande wao baadhi ya maafisa usafirishaji katika mabasi mbalimbali mkoani Njombe wamesema licha ya wao kuwaelimisha abiria namna ya kutumia vyombo vya moto vizuri ikiwemo kufunga mkanda wakati wa safari lakini wanaamini maadhimisho hayo yatatumika katika kuweka mkazo kwa abiria.
Kelvin Ndimbo ni Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Njombe ambaye amesema kuwa wamelazimika kusogeza mbele maadhimisho hayo kutokana Na muingiliano wa majukumu kwa mgeni rasmi ambaye ni mkuu wa Mkoa wa Njombe .
Kwa Upande Wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Wilbroad Mutafungwa Ameendelea Kusisitiza Utii wa Sheria za Barabarani Bila Usumbufu Wowote Ili Kuepusha Adha Inayoweza Kujitokeza.
0 comments:
Post a Comment