WAKILI WA SERIKALI MKOA WA NJOMBE YAHAYA MISANGO AKIZUNGUMZA
Imeelezwa Kuwa Kutokea Kwa Vurugu Na Kuvunjika Kwa Amani Kwa Baadhi Ya Maeneo Ya Uchaguzi Hapa Nchini Itasababishwa Na Tume Yenyewe Kwa Kushindwa Kutangaza Matokeo Sahihi Na Kwa Wakati Kutokana Na Baadhi Ya Wasimamizi Wa Majimbo Na Kata Kuwa Na Itikadi Za Siasa.
Kauli Hiyo Imetolewa Na Mratibu Wa Uchaguzi Mkoa Wa Njombe Hilmar Danda Wakati Akitolea Ufafanuzi Juu Ya Maoni Ya Viongozi Wa Taasisi Za Kidini Na Wadau Ambao Wamesema Uzoefu Unaonesha Kuwa Vurugu Za Kipindi Cha Uchaguzi Huanzia Kwa Wasimamizi Wenyewe.
Mratibu Danda Amesema Kipindi Hiki Cha Uchaguzi Watumishi Wa Serikali Hawapaswi Kushabikia Maswala Ya Kisiasa Kutokana Na Watumishi Hao Kupata Fursa Ya Kusimamia Vituo Vya Uchaguzi Na Hivyo Wanapaswa Kuzingatia Maadili Ya Utumishi.
Wakili Wa Serikali Mkoa Wa Njombe Yahaya Misango Amesema Sheria Inasema Matokeo Yanapaswa Kutangazwa Mara Tu Kukamilika Kwa Zoezi Ya Kupiga Kura Na Kusema Mwenye Mamlaka Ya Kutangaza Matokeo Ni Tume Ya Taifa Ya Uchaguzi Na Siyo Kila Kiongozi Wa Serikali.
Kwa Upande Wao Wananchi Mjini Njombe Wamesema Kuwa Ili Vurugu Zisiweze Kujitokeza Katika Kipindi Cha Uchaguzi Ni Vema Tume Ikatenda Haki Kwa Vyama Vyote Na Kufuata Sheria Za Uchaguzi Kwani Mara Nyingi Tume Imekuwa Ikifanya Makosa Na Kutumia Nguvu Ya Dola
0 comments:
Post a Comment