Filikunjombe akiwasalimia wananchi wa mwambao wa ziwa Nyasa
wananchi wa jimbo la Ludewa wakimpokea Filikunjombe kwa shangwe na ndelemo
Mgombea
ubungea wa jimbo la Ludewa katika mkoa wa Njombe kupitia tikeati ya chama cha
mapinduzi(CCM) Bw.Deo Filikunjombe amepita bila kupingwa wilayani hapa baada ya
mgombea wa chama cha demokrasia na
maendeleo(CHADEMA) kushindwa kutimiza
masharti na taratibu za ujazaji wa fomu za kuwania nafasi hiyo.
Msimamizi wa
uchaguzi wilayani Ludewa Bw.Wiliam Waziri alisema kuwa mgombea wa Chadema
alishindwa kutimiza taratibu za ujazaji wa fomu hizo hivyo kukosa sifa ya kuwa
mgombea wa ubunge hivyo kupelekea nafasi
hiyo kujazwa na mtu mmoja ambeye alimtangaza rasmi Filikunjombe kuwa mbunge
ambaye amepita bila kupingwa.
Bw.Waziri
alisema kuwa katika kinyang’anyilo hicho wagombea waliochukua fomu walikuwa
wakitokea vyama vinne ambavyo ni DP,TLP,CHADEMA na CCM hata hivyo wagombea
waliorudisha fomu ni wakutoka vyama vya CCM na CHADEMA ambapo hata hivyo mgombea
wa CHADEMA alishindwa kurejesha fomu ya kiapo cha maadili ya sheria za uchaguzi
na kupelekea kukosa sifa za kupitishwa
kuwa mgombea.
Alisema kuwa
mgombea huyo wa chadema ambaye alimtaja jina kuwa ni Bathromeo Mkinga alitakiwa
kutoa maelezo ya kwanini aliondolewe katika kinyang’anyilo hilo lakini
alishindwa kutoa maelezo yanayojitosheleza na kuishawishi tume hivyo kupelekea Filikunjombe kupita bila
kupingwa.
“Namtangaza
Bw.Deo Filikunjombe kuwa mbunge aliyepita bila kupingwa katika jimbo la
uchaguzi la Ludewa kutokana na mgombea
wa chadema kushindwa kukamilisha taratibu na masharti katika fomu na kushindwa
kutoa maelezo kwa maandishi yaliyonyooka hivyo kama msimamizi wa uchaguzi namtangaza
rasmi Bw.Filikunjombe kuwa mbunge wa jimbo la Ludewa”,alisema Bw.Waziri.
Bw.Waziri
amewataka wananchi wa wilaya ya Ludewa kuwa watulivu na wenye busara katika
kipindi hiki cha uchaguzi kwani kama wilaya ya Ludewa ilivyozoeleka kwani kabla ya uchaguzi kulikuwa na maisha na baada
ya uchaguzi kunamaisha hivyo hakuna haja ya kurumbana wakati wa kampeni za
kuwasaka madiwani ili kulinda amani ya Taifa.
Hata hivyo
wananchi wa wilaya ya Ludewa walisema kuwa hiyo ni laana inayowapata wapinzani
kutoka kwa wazee wa Ludewa kwani awali wazee wa wilaya hii walionya kuwa
hawahitaji mtu mwingine kugombea na atakayediriki kufanya hivyo wao
watamshughurikia kikamilifu kutokana na Filikunjombe kuwafanyia makubwa
wananchi wa jimbo lake.
Akieleza
hayo mmoja wa wananchi hao Bw.Timoth Komba alisema kuwa kutokana na utendaji wa
Filikunjombe wanaludewa hawakuwa na haja ya kuwa na watu wanaompinga mbunge wao
hivyo yaliyowakuta Chadema wilayani hapa ni laana za wazee ambao walishatoa
angalizo mapema kabla hata ya mchakato wa kura za maoni.
Aidha
aliwataka wananchi wengine kuacha malumbano yasiyo ya msingi na kuendelea na
shughuri zao za kujiingizia kipato kwani tayari mbunge amejulikana na mchakato
wa kuwasaka madiwani ukiendelea hivyo kufanya uchaguzi usio na vurugu hasa
katika kata ambazo zimewasimamisha wagombea wa udiwani wa vyama vya upinzani.
Mwisho.
0 comments:
Post a Comment