Mgombea urais kupitia umoja wa Katiba ya Ukawa amezuiwa kutumia uwanja wa Jangwani kuzindua kampeni yake iliyotarajiwa kunyika siku ya jumamosi ijayo.
Kwa mujibu wa barua iliyotolewa na Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala ya terehe 25 Agosti imebainisha kuwa ombi la Ukawa kufanyia mkutano katika uwanja huo limezuiwa kufuatia uwanja huo kuwa na matumizi na mwombaji Mwingine ambaye hajatajwa katika barua hiyo huku barua hiyo ikiwashauri kutafuta eneo lingine kufanyia uzinduzi huo.
Hii ni mara pili kwa Umoja huo kuzuiwa kufanyia kampeni yake kufuatia kukatazwa uwanja wa Taifa na hatimaye Jangwani leo.
Uwanja wa Jangwani ulitumika kuzindua kampeni za Chama cha Mapinduzi (CCM) ambapo maelfu ya wananchi walijumuika kushuhudia uzinduzi wa kampeni hiyo ambayo inadaiwa kuwa ni kihistoria tangu chama hicho kianze masuala ya kisiasa nchini Tanzania.
Barua ya zuio la Lowassa kuzindua kampeni Jangwani
0 comments:
Post a Comment