Msanii wa filamu nchini Tanzania, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ amewachana wasanii kwa kuwaita wanafiki kutokana na kuukacha uzinduzi wa kampeni za Chama cha Mapinduzi (CCM) uliofanyika katika Uwanja wa Jangwani wiki iliyopita.
Akihojiwa amedai kuwa anashangazwa kuona baadhi ya wasanii wenzake wameikacha CCM na kuupigia debe Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) wakati serikali ya CCM imewafanyia mambo makubwa.
Amesema kuwa wasanii ni wanafiki na ndiyo maana wakati mwingine wanatakiwa kuambia ukweli tu kwani serikali ya CCM imewafanyia mambo mengi kwenye sanaa na ndiyo maana siku za hivi karibuni walimuaga kwa kishindo rais Jakaya Kikwete.
Ameongeza kuwa sasa anashagaa baadhi ya wasanii waliokuwa nao katika hafla hiyo nao wanaiponda CCM na kushabikia Ukawa ambao leo wanazindua kampeni za urais jambo ambalo kwa upande wake ameliita ni unafiki.
0 comments:
Post a Comment