Uzinduzi huo umekuwa wa aina yake kufuatia kuwa na shamra shamra nyingi na za aina yake kuanzia jana siku ya ijumaa ambapo inadaiwa baadhi ya wananchi walilazimika kulala katika viwanja vya Jangwani kusubiri uzinduzi huo.
Akizungumza katika mkutano huo Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe amesema kwamba wamezindua kampeni zao leo ili kuhakikisha kuwa wanawapa wananchi mabadiliko wanayo yataka ambayo yataleta maisha mapya kwa watanzania.
Amesema kuwa umasikini sio sifa, wala wao katika umoja wa UKAWA hawatamani umasikini, wakati wa kuamini viongozi masikini hapana. wanataka Tanzania iondoke katika umasikini kwa sababu umasikini ni laana.
“Nimalizie kusema kwa nini Lowassa, sisi tulifanya tafiti, kwa sababu taifa letu limeendeshwa kwa propaganda kwa muda mrefu, Lowassa kwa muda wa miaka 10 amekuwa muhanga wa propaganda za CCM.”Amesema Mbowe.
Naye Fredirick Sumaye amesema ametoka chama cha mapinduzi, katibu mkuu alisema wao ambao hawatukuteuliwa hatukuwa na maadili, amesema kama kipimo cha maadili ni mheshimiwa Kinana yeye atakuwa mtakatifu.
Amesema leo Lowassa ametoka CCM ameonekana hafai, lakini ni Kikwete ndiye aliyemfanya waziri mkuu wake, kuna Rais anaweka kiongozi ambae hafai? Lakini ni Lowassa huyuhuyu ndiye aliyemuingiza Kikwete Ikulu.
Kwa upande wake mgombea Urais wa UKAWA Lowassa amesema sera yake itakuwa Kipengele cha kwanza elimu, cha pili elimu na cha tatu elimu. Maneno haya ameyaazima kwa waziri mkuu wa Uingereza. Cha kwanza elimu itakuwa inagharamiwa na serikali kuanzia darasa la kwanza mpaka chuo kikuu.
Eneo la pili la kilimo ili tuweze kutengeneza ajira za kutosha na eneo la tatu ni kuweka umuhimu afya iwe bora kwa akina mama na watoto wadogo.
0 comments:
Post a Comment