MGOMBEA
urais wa CCM Dr John Magufuli amempongeza mbunge wa jimbo la Ludewa Deo
Filikunjombe kwa kupita bila kupingwa huku akiahidi Neema kwa wakazi wa
Mlangali kuwa ahadi Yake ya kwanza ni barabara ya lami na maji.
Mgombea
huyo wa Urais alitoa kauli hiyo leo kwa nyakati tofauti wakati
akizungumza na wananchi wa Mavanga na kata ya Mlangali wakati wa kampeni
zake za kutafuta ushindi wa CCM
Alisema
kuwa shida za watanzania si vyama Bali kutatuliwa matatizo Yao na kuwa
yeye atakuwa Rais wa vyama vyote bila kujali itikadi zao
Hivyo
alisema iwapo ataingia ikulu kwanza kwa wakazi wa Ludewa ataanza na
barabara ya Lami pia umeme wa uhakika na Huduma ya maji ikiwa ni pamoja
na elimu bure kutoka shule ya msingi hadi sekondari kidato cha nne .
Alisema
kuwa kikubwa anachojivunia kwa mbunge wa Ludewa Bw Filikunjombe ni
uchapakazi wake hivyo kwa pamoja wananchi wakichagua CCM kwa ngazi zote
tatu ni uhakika maendeleo yatasonga mbele .
Dr Magufuli alisema kuwa akiwa Ikulu atahakikisha serikali Yake inakuwa na mawaziri watendaji wachapakazi na si vinginevyo
0 comments:
Post a Comment