Mvutano wa kisiasa baina ya pande mbili zenye misimamo tofauti kisiasa nchini Tanzania, UKAWA na CCM wakati huu wa kampeni umehamia kwenye nyimbo za muziki hasa wa bongo flava.
Nyimbo za wasanii mbalimbali zinazozungumzia vyama hivyo vya siasa na nyingine kuwataja majina wagombea Urais kwa tiketi ya vyama hivyo zimekuwa vivutio kwa wananchi kwa kuongoza kwa Downloads tofauti na nyimbo nyingine ambazo sio za kisiasa.
Nyimbo zinazoongoza kwa kupakuliwa na kusikilizwa zaidi ni pamoja wimbo wa msanii chipukizi Snaida unaoitwa ‘Ukawa’ yenye dowloads zaidi ya elfu 48 ikifuatiwa na ile ya Diamond Platnumz inayoitwa ‘CCM No-1’ iliyofikisha dowloads zaidi ya elfu 45.
Nyimbo nyingine za kisiasa zinazofanya vizuri ni pamoja na ngoma ya Nay wa Mitego iitwayo ‘Lowassa’ ikiwa na downloads zaidi ya elfu 23 na ile ya D-Manyuti inayoitwa ‘Magufuli’.
Aidha nyimbo za siasa zimeanza kufanya vizuri tangu zamani kipindi cha mchakato wa kupata mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi.
0 comments:
Post a Comment