Mgombea
Urais kwa Tiketi ya CCM John Pombe Magufuli akimsikiliza Deo
Filikunjombe, Mbunge wa Ludewa kueleza matatizo
yanalolikabili jimbo hilo
Katikati
ni John Pombe Magufuli mgombea Urais CCM, Kushoto ni Deo Filikunjombe
aliyepita bila kupingwa Jimbo la Ludewa, na kulia ni Khamis Kayombo
mgombea udiwani CCM Kata ya Mlangali
Mbunge wa Jimbo la Ludewa, Deo Filikunjombe aliyepita bila kupingwa akizungumzia jimboni humo akisisitiza jambo
Waziri wa nyumba, ardhi na makazi, Willium Lukuvi akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo.(P.T)
Katika
hali iliyotegemewa na wengi Wilayani Ludewa ya kuungwa mkono kwa mgombea
Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM Dkt John Pombe Magufuli
imejidhihirisha hii leo katika uwanja wa mpira wa miguu Ludewa baada ya
wananchi kujitokeza kwa wingi kumlaki mgombea huyo.
Akizungumza
wakati wa mkutano huo Magufuli alimpongeza mbunge aliyepita bila
kupingwa katika jimbo hilo Deo Filikunjombe, kutokana na washindani
wengine wa vyama vya upinzani kushindwa kukidhi vigezo.
Magufuli
ameingia Wilayani Ludewa akitokea Wilaya ya Songea Vijijini Jimbo la
Madaba huku akiongozana na aliyekuwa Waziri wa ardhi, Nyumba na Makazi
ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Isimani, Willium Lukuvi.
Magufuli
amesema kuwa Filikunjombe ni mfano wa kuigwa na anastahili kuendelea
kuwa mbunge wa Jimbo la Ludewa kutokana na kazi kubwa aliyoifanya
Wilayani Ludewa kwa kushirikiana na wananchi katika kuhakikisha shughuli
za maendeleo zinasonga mbele.
Sawia na
hayo ameeleza kuhamasika na utendaji kazi wa mbunge huyo huku akimuita
kuwa ni mwamba wa Ludewa ambapo alimtaka kueleza matatizo yanalolikabili
Jimbo hilo ikiwa ni pamoja na barabara huku akimuahidi kuzifanyia kazi
haraka iwezekanavyo.
Akizungumza
katika mkutano wa awali uliofanyika katika kitongoji cha Mgombezi, Kata
ya Mavanga, Filikunjombe alisema kuwa wananchi wake wanakabiliwa na
tatizo la maji, umeme na barabara ya lami ambapo ni pamoja na ile
itokayo Njombe hadi Ludewa.
Hata
hivyo Filikunjombe amemuahidi ushindi wa kishindo kwani wananchi wake
wana imani kubwa na Chama Cha Mapinduzi CCM hivyo wanachama wa CHADEMA,
CUF na vyama vingine vya upinzani watampatia kura nyingi na imani yake
kubwa kwamba Wilaya hiyo itaongoza Kitaifa kwa ushindi mkubwa.
"Umekuwa
waziri wa ujenzi umetusaidia barabara mbalimbali tunakupongeza lakini
tunaomba pia utusaidie barabara ya lami Kutoka Njombe kupitia Malangali,
Ludewa mpaka Manda hivyo ikiwa kwa kiwango cha lami utakuwa umetatua
changamoto kubwa na muhimu kwa wananchi" Alisema Filikunjombe
Magufuli
amefikia hatua ya kumuita Mbunge huyo kuwa ni Magufuli ajaye kutokana na
uwezo wake mkubwa wa utendaji kazi ambao umejidhihirisha Jimboni kwake
na Tanzania nzima huku akijilinganisha naye kwani Tanzania inamfahamu
vyema akiwa akiwa serikalini hususani Wizara ya Ujenzi.
Wakati huo huo alisema kuwa serikali ya awamu ya tano haitakuwa serikali ya lelemama kwani watendaji atakao wachagua ikiwa ni pamoja na mawaziri watakuwa ni wachapakazi na endapo kama watachelewesha maendeleo wataisoma namba.
Wakati huo huo alisema kuwa serikali ya awamu ya tano haitakuwa serikali ya lelemama kwani watendaji atakao wachagua ikiwa ni pamoja na mawaziri watakuwa ni wachapakazi na endapo kama watachelewesha maendeleo wataisoma namba.
Aidha
Magufuli alisema kuwa serikali ya tano itakuwa ya watu makini
wanaosimamia wananchi wake na kuwapenda ili kuweza kufanya kazi kwa
makini na utatu uliotukuka kwani shida za watanzania anazifahamu vizuri
hazisomi kwenye kitabu wala hahitaji kusimuliwa na mtu yeyote.
Magufuli
amewahakikishia wananchi kuwa ilani ya CCM imeelekeza vyema kuhusiana na
mikopo ya wananchi ambapo kila kijiji kitapewa milioni 50 ili kutoa
mikopo iliyo nafuu na kuwafanya wananchi wote kuweza kukopa na kukuza
kipato chao cha kila siku.
"Natamka
hadharani serikali yangu wanafunzi watasoma bure kuanzia darasa la
kwanza hadi kidato cha Nne kwani inawezekana kwa sababu tayari wezi
wachache wamekwisha anza kukimbia hivyo nitawanyoosha wote na kudhibiti
ubadhilifu wa fedha unaobwinywa na wachache" Alisema Magufuli
Amesema
alipokuwa waziri alikuwa anatumwa kufanya kazi lakini sasa atakuwa
anawatuma viongozi wote ambao atawateuwa huku akieleza wazi kupita kwa
Filikunjombe bila kupingwa kwa mara ya pili sasa ni kama yeye alivyopita
Jimbo la Chato mara mbili bila kupingwa.
"Nimalize
kwa kuwaomba wana Ludewa wote kuchagua diwani, Mbunge na Rais wa CCM
ili maendeleo yaweze kutekelezwa kwa kasi" Alimaliza Magufuli
Akiwa
njiani kuelekea Wilayani Ludewa, Magufuli amefanya mikutano zaidi ya
Mitano kwa siku moja huku baadhi ya maeneo wananchi wakizuia msafara
kutaka walau awasalimie
0 comments:
Post a Comment