Waziri wa zamani wa Elimu, Joseph Mungai ametangaza kukihama chama Chama Mapinduzi na kuhamia umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).
Mungai ametangaza uamuzi huo katika mkutano wa hadhara wa kampeni za UKAWA katika Uwanja wa Shule ya Msingi Wambi, wilayani Mufindi mjini Mafinga.
Mungai aliwahi kuwa mbunge kwa miaka 35 kupitia CCM na aliweza kuteuliwa nafasi mbalimbali za uwaziri ikiwamo Wizara ya Kilimo, Mambo ya Ndani na Wizara ya Elimu.
Katika mkutano huo Mungani alimnadi mtoto wake ambaye ni Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mafinga Mjini kupitia Chadema, William Mungai ambapo alisema wananchi wa jimbo hilo wanatakiwa kumchagua William Mungai kwa sababu mbunge aliyemaliza muda wake katika jimbo hilo hakuweza kuongoza kama alivyofanya yeye.
0 comments:
Post a Comment