Mgombea
Ubunge Jimbo la Ludewa kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema), Msambichaka Mkinga (kushoto), akizungumza katika mkutano na
waandishi wa habari Dar es Salaam , wakati akipinga kupitishwa bila
kupingwa mgombea mwenzake wa jimbo hilo kupitia Chama Cha Mapinduzi
(CCM), Deo Filikunjombe na kudai kulikuwa na hujuma. Kulia ni Wakili
wake, Paulo Kalomo.
Mgombea
Ubunge Jimbo la Ludewa kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema), Msambichaka Mkinga, akionesha fomu namba 10 ambazo alikabidhi
kwa Msimamizi wa Uchaguzi.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Na Barnabas Njenjema.Ludewa
MGOMBEA
Ubunge wa Jimbo la Ludewa kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema), Msambichaka Mkinga amepinga vikali kupitishwa bila kupingwa
mgombea mwenzake wa jimbo hilo kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Deo
Filikunjombe na kudai kulikuwa na hujuma.
Mkinga
alitoa malalamiko hayo mbele ya waandishi wa habari Dar es Salaam leo
asubuhi na kueleleza kuwa sababu zilizotolewa na msimamizi wa uchaguzi
wa jimbo hilo kuwa hakupeleka fomu namba 10 hazikuwa na ukweli wowote.
"Nilipofika
ofisi ya msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Ludewa nilisaini na kukabidhi
tamko la kuheshimu na kutekeleza maadili ya uchaguzi ya mwaka 2015 (fomu
namba 10) na baada ya kusaini nilimkabidhi msimamizi wa uchaguzi pamoja
na fomu namba 8B,picha, stakabadhi ya malipo ya dhamana ambapo
vilihakikiwa na Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi, Gervas Lupembe" alisema
Mkinga.
Mkinga
alisema katika jambo lisilo la kawaida msimamizi wa uchaguzi wa jimbo
hilo hilo hakubandika kwenye ubao wa matangazo tamko hilo na alipomfuata
msimamizi huyo kumuulizia msaidizi wake Lupembe alikiri kupokea na
kuziwasilisha kwa kiongozi wake ili kutia saini ambaye naye alikiri
kuzipokea lakini wakati ana bandika tamko hilo la Mgombea wa CCM fomu
hiyo hakuiona.
Alisema
katika pingamizi alilowekewa dai mojawapo ni kutokuwepo tamko hilo
kwenye fomu zake hali inayoonesha wazi kuwa kulikuwa na mchezo mchafu
uliofanyika ili kumpitisha Filikunjombe bila kupingwa.
Mkinga
alisema kuwa kuwaondoa wagombea kwa sababu zisizo za msingi ni kuiminya
demokrasia na kuirudisha nchi nyuma kwani kunaweza kusababisha kukosa
viongozi wazuri na kubakia na viongozi wasiofaa na wasiotaka
kushindanishwa kwa kuwapa nafasi wananchi ya kumchagua kiongozi
wanayemtaka.
Mgombea
huyo alisema kutokana na sintofahamu hiyo alimuomba msimami wa uchaguzi
wa jimbo hilo kutupiliambali pingamizi lililotolewa dhidi yake na
mgombea mwenzake ambapo anasubiri majibu baada ya kuandika barua ya
malalamiko.
0 comments:
Post a Comment