Walemavu wa ngozi kuitikisa Ruvuma kwa maandamano

Maandamano makubwa kupinga mauaji pamoja na unyanyasaji dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino) yanatarajiwa kufanyika mkoani Ruvuma machi 2 mwaka huu. Kwa mujibu wa katibu mtendaji wa chama cha walemavu wa ngozi mkoa wa Ruvuma, Amini Mapunda amesema kwamba lengo la maandamano hayo ni kuishinikiza serikali kuwachukulia hatua kali wote waliohusika na kubainika na tuhuma za kuhusika na mauaji ya albino kwa madai kwamba baadhi yao wamekamatwa lakini mwenendo wa kesi zao bado haueleweki. Mauaji ya Albino pamoja na wazee nchini Tanzania yamekuwa yakihusishwa na imani za kishirikina, utajiri ama nafasi mbalimbali za kisiasa kwa imani za kishirikina huku serikali ikishindwa kuchukua hatua kali kwa wahusika suala linalopelekea mauaji hayo kuendelea. Kwa upande wake mwenyekiri wa shirika la ROA, Mathew Ngalimanayo amesema kuendelea kwa mauaji hayo inatokana na jamii kukosa hofu ya mungu na wakati mwingine familia husika zikihusika kutokana na hali ngumu ya maisha hivyo kushawishika kirahisi.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: