CHADEMA KUUNGURUMA LUDEWA MKOA WA NJOMBE

CHADEMA KUUNGURUMA LUDEWA MKOA WA NJOMBE Chama cha demokrasia na Maendeleo chadema kimesema kuwa licha ya kuendelea kuwaelimisha wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura, chama hicho pia hakitasita kuzungumzia changamoto zinazojitokeza wakati wa zoezi hilo Kauli hiyo imetolewa na naibu katibu mkuu wa chama hicho Bara Mh. John Mnyika mara baada ya ufunguzi wa zoezi la kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura lililofanyika kitaifa makambako mkoani Njombe Mnyika amesema wanaipokeaa kwa mikono miwili kauli ya mwenyekiti wa Tume ya taifa ya uchaguzi kuwa vyama viwahamasishe wananchi kujiandikisha, na wao watazidi kufanya hivyo kwa kadri ya uwezo wao. Pia ameongeza kuwa tarehe 26 ya mwez wa pili watakuwa wilayani ludewa kuanzia saa nne asubuhi na baada ya hapo wataelekea lugarawa ambapo napo watakuwa na mkuno wa hadhara; katibu wa chadema wilaya ya ludewa bw;Alflred Ndege ulaya anawahamasisha wananchi wote wilayani hapa kujitokeza kwa wingi kupata nafasi ya kumsikiliza john mnyika atayeambatana na wabunge mbalimbali kutoka kambi ya upinzani: Wakati huo huo Mwenyekiti wa tume ya taifa ya Uchaguzi (NEC) jaji mstaafu Damian Lubuva amesema teknolojia mpya ya kuboresha daftari la kudumu la wapiga kura ni kwa ajili ya uandikishaji tu na halitatumika katika upigaji kura wala kuhesabu Akizungumza wakati wa uzinduzi wa uboreshaji wa daftari hilo la wapigakura mjini Makambako mkoani Njombe jaji Lubuva amewataka wadau mbalimbali kuhamasisha wananchi kushiriki kwa wingi katika zoezi hilo la kujiandikisha lililoanza jana Amesema kwamba zoezi lililoanza mkoani Njombe limekwenda vizuri kwa lengo lililowekwa kuvukwa hali iliyoonesha kwamba zoezi hilo litafanikiwa vizuri
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: