Akamatwa kwa kutoroka jela baada ya miaka 37 kupita

Mwanamke mmoja Kaskazini mwa Carolina, nchini Marekani, Chery, amekiri kuishi na mume wake maisha ya ndoa kwa zaidi ya miaka 30 bila kujua kuwa ni mfungwa aliyekimbia gerezani baada ya kuiba katika benki hali iliyompelekea kuwa muumini mzuri katika kanisa lake. Cheryl, amesema kuwa katika ndoa yake na mume wake Bobby, walifanikiwa kupata watoto wanne na waliishi maisha ya upendo na amani wakiendelea kuhudumia kanisa lao na kusambaza upendo. Amesema kuwa, wakati wanapitia kipindi kigumu mume wake alikuwa akifanya kazi mbili tofauti na kumfanya muda wake wa kupumzika kuwa mdogo ili kuweza kuisaidia familia yake na kuongeza kuwa mume wake alikuwa na aibu sana kwa wageni. Katika kipindi cha miongo mitatu aliweza kuhisi kuwa mume wake alikuwa na kitu anamficha kutokana na muda ambao anamhitaji kuwa karibu naye alikuwa akijivuta na kuwa mbali nae jambo ambalo lilimpa wasiwasi. Amesema Bobby alikuwa mpole, mcha Mungu na msiri sana bila kujua alikuwa mafichoni kwa muda wa mika 37 tangu alipotoroka katika jela Kaskazini mwa Carifonia, nchini Marekani, mwaka 1977 ambapo hadi anakamatwa alikuwa na umri wa miaka 64.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: