RATIBA ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara imeendelea kubadilika badilika kama hali ya hewa, baada ya jana Shirikisho la Soka nchini (TFF) kutoa ratiba nyingine, inayoonyesha vigogo Simba na Yanga watamenyana Machi 8, mwaka huu.
Tangu kupanguliwa kwa ratiba ya Ligi Kuu kupisha michuano ya Kombe la Mapinduzi Januari mwaka huu visiwani Zanzibar, ratiba ya ligi hiyo imekuwa haieleweki tena kutokana na baadhi ya timu kuwa na mechi za viporo.
Mechi mbili za kila timu ya Azam, Yanga SC, Mtibwa Sugar na Simba zilisimamishwa ili timu hizo ziende Zanzibar na hata baada ya kurudi zimeshindwa kumalizia viporo vyao haraka kutokana na sababu mbalimbali.
TFF ilipanga ichomeke mechi hizo katikati ya wiki ya mechi za timu hizo, ili ndani ya wiki mbili ziwe zimekwishacheza viporo hivyo, lakini ikashindikana.
Wakati mwingine timu ambayo ilitakiwa kucheza na timu iliyokuwa kwenye Kombe la Mapinduzi katika wiki husika ilikuwa ina mechi mkoa wa mbali.
Na ziara ya Azam FC Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ikasababisha mechi zao kusogezwa mbele pia.
Lakini inawezekana marekebisho haya ya ratiba ya Ligi Kuu yakawa ya mwisho kwa msimu huu, kutokana na TFF yenyewe kujiridhisha kusimamisha mara kwa mara mechi za michuano hiyo kunapunguza msisimko na ladha ya kimashindano.
Ligi Kuu inatarajiwa kuendelea keshokutwa kwa mechi kati ya Azam FC na Ruvu Shooting Uwanja wa Azam Complex, Chamazi na Yanga na Prisons Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment