KakaMkulu wa Kaya, salaam nakusalimia,
Nasema kuwa huru si rahisi kama ilivyo si rahisi kuwa rais na sasa Chokoraa nawasalimia. Kubadili majalala huku kuna siku nitaingia kwenye jalala la tindikali naapa kwa jina la bibi yangu mzaa mama yangu Shida wa Matatizo msinihusishe. Nasema msitake niseme kwa mtiririko maana yaliyonijaa kwenye koo ni mengi na njia ya ama kuyameza ama kuyatema ni ndogo na hivyo wacheni niyatapike liwalo na liwe maana ni bora moja kuliko sifuri na humu miye nahusikaje!?.
Kwani nani kaiona ramani ya kaya yetu, ile ramani halisi ya Danganyika ya Wadanganyika tuliyoachiwa na wazee wetu kabla haijabadilishwa na hawa wenye kujitangazia uhuru kila uchao kisa “uhuru na haki za raia” na mimi nauliza ni nini uhuru na haki za rais na kwa hili mnitoe maana simo.
Kaka mkulu wa kaya, nimetumwa na wadogo zangu akina Muuza Mayai na Karanga, na hata mama yangu mdogo Mama Ntilie kanituma nikusalimie.Hawa wawili wanasema wanakumbuka kabla ya kufariki baba wa kaya yetu na kabla ya wewe kuteuliwa na kikao kilichopita cha ukoo kuwa Mkulu wa Kaya na kuongoza kundi la akina kaka Muishiwa wa Maadili na Kiongozi Mbadhilifu katika kuiwakilisha kaya yetu hii, tulikuwa sisi wote ni wamoja watoto wa mzee Mdanganyika Mlipakodi na mama yetu Bi Mzalendo.
Ati wanasema baada ya kufariki baba yetu, kundi lenu likiongozwa na akina kaka Muishiwa walimpendekeza kaka yenu mkubwa Mtukutu kutuelekeza kule yalikofichwa maisha tarajari ya kaya yetu na ati baada ya siku chache kaka yetu huyu kujitangaza kuwa ‘Mtukufu’ watu wakaogopa lakini kwa vile ati kilikuwa kizazi kilicholelewa vyema na marehemu baba yetu kwa kutohoji yale yafwanywayo na wale wenye kuvaa lile joho lefu la baba na wenzake lenye rangi ya Kiongozi, basi wakakaa kimya. Hata hivyo yale yaliyotendeka ati yalitendeka na hata akina Mlalahoi wakaanza kujenga maghorofa kwa kuuza vitunguu swaumu nisikuchoshe na historia, salaam nakusalimia.
Baadaye ndipo kijiti alipopewa kaka mkubwa Muishiwa. Wanasema ati huyu naye kwa sehemu alizingatia sehemu ya mafunzo ya marehemu mama yetu Mzalendo binti Mdanganyika ijapokuwa ni kweli kwamba yeye kijiko chake kilikuwa kikubwa maakulini ukizingatia na sisi wengine, lakini walau alijenga daraja na siyo ukuta, nasema nisikuchoshe ila salaam nakusalimia.
Sasa kuna Yule dada yetu mkubwa ambaye hasa ndiye aliyenifanya nikuandikie waraka huu hasa kwa vile binafsi naweza nisipate nafasi ya kuonana na wewe mwaka huu, si kwa sababu sipendi ama ati kwa vile naogopa wale walinzi wako kama mjomba, lah! Bali kwa vile lile daraja kutoka huku kwetu kuja huko kwenu lina mushkeli kidogo hasa baada ya juzi tu wadanganyika kuchoshwa na kuamua kutenda watendavyo mradi iwe iwavyo, salaam nakusalimia.
Nasema watu wakichoshwa ni heri ya punda mzee kubeba mzigo yeye na mwana kuliko mtu ama aliyeshiba mema au asiyekula kabisa maana wote huwa na wazimu kwa sababu tofauti na mimi humu sihusiki.
Dada yetu mkubwa Mjasiriamali ameniagiza nikusalimie na kisha nikueleze kwamba kwake yeye ijapokuwa hapendi hata kidogo jinsi ati unavyotuhumiwa kwa mjomba na shangazi kuwa na sauti nzito kuliko wewe kwenyekaya yetu, lakini walau alikuwa bado angali na imani na ile “Siri kali” labda kwa vile ilikuwa imefichwa na haikujulikana kwake na hivyo si kwamba aliiamini “Siri kali” bali aliamini kwamba kuna siku na yeye atakuwa sehemu ya wale wenye kuifahamu siri hiyo ifichwayo kwa udi na uvumba na hilo linanifanya salaam nakusalimia.
Anasema baada ya hivi majuzi watu wasiojulikana kujitangazia mamlaka bila madaraka na kuufunga mji wa Mtwara tena pasina kupata upinzani wowote kutoka kwa walinzi wa “Siri kali”, dada yangu mjasiriamali amejiuliza maswali kadhaa ambayo machache yake amenitaka nikuulize na mimi sasa nakuuliza; Hivi ni kweli kwamba ile “Siri kali” yetu imevuja na sasa kila aliyeko nje anaona ndani kama aliyeko ndaniaonavyo nje!? Nasema usijesema miye sina adabu ninazo tena tele lakini najiuliza inawezekanaje kwamba genge la “wahuni” linafunga mji kiasi Chokoraa wa Muhangaikaji wa Mlalahoi wa Pangupakavu wa Kabwela wa Mdanganyika na hata dada yangu chakaramu Mjasiriamali hatuwezi kutoka ndani na kwenda kuokoteza mkate wa siku? .
Samahani unisamehe, si hoja yangu ya msingi ikiwa ni sahihi kwako kujenga njia ya panya na kupitisha gesi, oil ama mafuta hiyo kwangu si hoja. Nasema yafaa nini mimi kuhoji ikiwa hilo ni sahihi ama si sahihi ikiwa mimi Mdanganyika sina haki wala hadhi ya kuhoji usahihi ama tafsiri ya usahihi wenyewe?.
Kinachonikera mimi na dada yangu Mjasilia ni kwanini na hasa inawezekanaje kwamba ‘watu wasiojulikana’ wanaweza kufunga mji na biashara zake zote na hadi sasa wakawa bado “hawajajulikana”?.
Ati! Utani wa kuniambia tena ati ni “kundi la wahuni” wanaohatarisha maisha ya wadanganyika wa Ntwara tafadhali tuuacheni maana wahuni hawa sasa wamepevuka mno kutoka daraja la kawaida la uhuni sasa wanaelekea kuwa ‘waahini’ na mimi humo sihusiki. Hivi inawezekanaje kwamba watu ‘wasiojulikana’ ama “wahuni” kama ambavyo baadhi yenu
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment