MAN UNITED YATINGA ROBO FAINALI KOMBE LA FA, SASA KUIVAA ARSENAL
MANCHESTER United imetoka nyuma kwa bao 1-0 na kushinda 3-1 hivyo kutinga Robo Fainali ya Kombe la FA dhidi ya Preston Noth End usiku huu na sasa watakutana na mabingwa watetezi, Arsenal.
Scott Laird alitangulia kuwafungia wenyeji, Preston dakika ya 47 akimtungua kwa shuti la kubabatiza kipa David de Gea, kabla ya Ander Herrera kuisawazishia United dakika ya 65 akifumua shuti lililowapita mabeki wa Preston na kipa wao.
Marouane Fellaini akaifungia bao la pili Manchester United dakika ya 72, kabla ya Wayne Rooney kusababisha penalti dakika za lala salama na kwenda kufunga mwenyewe
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment