MWENYEKITI wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kata ya Kilondo wilaya ya Ludewa mkoani Njombe ashauri wananchi wanaokwamisha jitihada za maendeleo zinazofanywa na mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe (CCM) kuchapwa fimbo .
Mwenyekiti huyo BwEdgar Kyullaalitoa agizo hilo mbele ya mbunge Filikunjombe na wananchi wa kijiji cha Kilondo wakati wa mkutano wa hadhara wa ulioambatana na uzinduzi wa mradi wa umeme wenye thamani ya zaidi ya Tsh milioni 300 uliofadhiliwa naWakala wa Umeme Vijijini (Rea) na kusimamiwa nakampuni za Renewable Energy Technology Development (Retdco) na Kilondo Investment.
Alisema kuwa jitihada zinazofanywa na mbunge Filikunjombe katika jimbo la Ludewa ni kubwa na za kupongezwa na si za kubezwa na mtu yeyote ama chama chochote za siasa katika jimbo hilo .
" Mbunge wetu anafanya kazi kubwa sana katika kutuletea maendeleo wananchi wa Ludewa bila kuangalia itikadi za vyama vyetu na ni wabunge wachache sana wenye moyo kama wa Filikunjombe ombi langu tuungane pamoja katika masuala ya maendeleo wapo wachache wetu ambao wanatangulia itikadi za vyama hata katika mambo ya maendeleo sasa kama mwenyekiti wa Chadema nashauri viboko vitumike kwa wapinga maendeleo bila kujali vyama vyao na mimi nitaongoza zoezi la kuwakamata wote wanaopinga maendeleo hapa kijijini kwetu " alisema mwenyekiti huyo wa Chadema
Bw Kyulla alisema wakazi wa Ludewa wanatambua kwamba mradi huo utakaolifanya eneo hilo kupata umeme kwa mara ya kwanza, umefanikiwa kupitia jitihada binafsi za Mbunge Filikunjombe
Chadema ambacho awali hakikuwa na nguvu kubwa Ludewa, kimefanikiwa kushinda viti kadhaa vya wenyeviti wa vijiji na vitongoji na hivyo kujiongezea nguvu zake jimboni humu.
“ Ndugu zangu wananchi bila shaka mnanitambua vema kazi yangu , ninawaonya wote watakaojaribu kumhujumu mbunge wetu jembe mheshimiwa Filikunjombe katika utekelezaji wa mradi huu,tutaonana wabaya wote mnajua kuwa maendeleo haya hayana uhusiano wowote na itikadi bali ni kwa manufaa ya kizazi chetu na sisi wenyewe ni wabunge wangapi wamepita bila kuleta maendeleo Ludewa ila huyu kweli ni mbunge wa mfano kwetu lazima tuungana pamoja ,” alisema.
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Kilondo Investment Bw Eric Mwambeleko, alisema mradi huo uliwasilishwa Rea ukakataliwa kutokana na vigezo kadhaa, ndipo Filikunjombe alipoingilia kati na kufanikisha kupatikana kwa fedha za mradi.
Akizungumza na wananchi hao mbunge Filikunjombe alisema Chadema ni chama cha Watanzania wanaopaswa kuheshimiwa, lakini suala la kushika dola na kuchagiza maendeleo ya nchi, linabaki kuwa la CCM hivyo lazima wananchi kujenga umoja katika mambo ya maendeleo .
“Tuwaheshimu, tuwapende hawa wenzetu (Chadema) lakini tuhakikishe kwamba CCM inaendelea kushika dola na kuiletea nchi maendeleo,” alisema.
Hata hivyo, alisema jukumu hilo linapaswa kufanywa na wote wenye dhamana ya kuutumikia umma katika maeneo yao bila kujali nafasi zao katika jamii na kuwa si vibaya hata wazee kushiriki katika maendeleo kwa manma ya kwenda kushauri vijana wanapofanya kazi .
Pia aliwataka wakazi wa kata hiyo kushiriki kikamilifu katika kuchangia nguvu za umma kuwasaidia wataalam wanaoujenga mradi huo ili waweze kutekeleza kwa moyo mmoja badala ya kuwanyima ushirikiano .
Mradi huo unaojengwa kwenye maporomoko ya mto Kilondo, utazalisha umeme wa kilowati 50 kwa ajili ya matumizi ya wakazi wa kijiji cha Kilondo na baadaye Nsele vijiji ambavyo kimsingi bila mradi huo uwezekano wa kufikiwa na umeme wa Tanesco ni vigumu zaidi kutokana na Jografia ya eneo hilo la Mwambao mwa ziwa nyasa
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment