ELIMU YA MSAADA WA KISHERIA YAENDELEA KUWAOKOA WANANCHI WA KATA YA LUPILA MAKETE

Na eddyblog, Makete Wananchi wilayani Makete mkoani Njombe wametakiwa kujitokeza kupatiwa msaada wa kisheria, na wasaidizi wa kisheria waliopo wilayani hapo ili kuwasaidia kutatua migogoro mbalimbali inayowakumba kutokana na ukosefu wa elimu ya sheria Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa chama cha wasaidizi wa kisheria wilayani Makete PACEMA ambaye pia ni msaidizi wa kisheria kata ya Lupila Bw. Nebert Sigala wakati akizungumza na mwandishi wetu kuhusu elimu ya masuala ya kisheria katika kata hiyo Bw. Sigala amesema kwa hivi sasa wapo wananchi ambao wamekuwa wakijitokeza kupatiwa msaada wa kisheria ambao umekuwa ukiwasaidia katika matatizo yaliyokuwa yakiwakabili kwa kuwa hawakuwa na uelewa huo toka awali Ametaja baadhi ya maeneo ambayo yamekuwa yakihitajika zaidi na wananchi hao kuwa ni sheria za ardhi, sheria ya mtoto pamoja na sheria mbalimbali za nchi, jambo ambalo limewasaidia wananchi wa kata hiyo kuona umuhimu wa kumiliki ardhi kisheria
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: