KATIBA INAYOPENDEKEZWA YAGAWIWA KWA WANANCHI LUDEWA.

mkuu  wa wilaya mpya wa Ludewa Bw.Antony Choya

Na.barnabas njenjema

Ludewa

katiba inayopendekezwa ya jamhuri ya muungano wa tanzania imeanza kusambazwa kwa wananchi wa wilaya ya ludewa mkoa wa Njombe iliwawezekusoma na kuielewa.


Hayo yalisemwa na mkuu wa wilaya Bw.Antony Choya alipokuwa akitoa salaam kwa shirika la maendeleo Ludewa halimaarufu kama LUDESO wakati wa sherehe za uzinduzi wa tawi hilo wilayani hapa.

Akieleza juu ya katiba amewaasa wana LUDESO kupigia kura ya ndio katiba pendekezwa kutokana na ubora wake kwa wakati huu.

jumlya ya nakala 7800 zimeletwa kwa wilaya ya Ludewa ambapo zimetawanywa katika kila kata na kuomba wananchi kujitokeza kwa wingi kuisomana kuielewa katiba pendekezwa na sio kusimuliwa juu ya katiba hiyo. 

pia Bw.choya amewaomba wana ludewa kushirikiana naye pamoja na kamati yaulinzi na usalama wilaya ya ludewa katika shughuli mbalimbali  za maendeleo.

Mkuu wa wilaya ya Ludewa  ambaye hamia hivi sasa kwaniaba ya Juma Madaha hakuwa mbali kumpa sifa za utendaji wa kazi na kuwajibika kwa wananchi Mh.deo filikunjombe  mbunge wa jimbo la Ludewa.

''nawapongeza kwa kuchagua mtu anayependa maendeleo ya Ludewa kwa hilo nawapa sifa ilakamwe msimpoteza ''alisema Bw.Choya.

pia ameeleza kuwa ameshafanya kazi na mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Ludewa Bw.stanley Kolimba wakati akiwa mbunge wa jimbo la Ludewa pamoja na mkuu wa wilaya,

''nashukuru kuja ludewa na nimeonana na watu niliowazoea na naahidi nitafanya nao kazi vizuri kadriniwezavyo kwa kuwa nipo na mwenyeji wangu tunayefamihana vizuri''alisema mkuu wa wilaya mpya wa Ludewa

Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: