SIMBA SC KAZI WANAYO KWA PRISONS LEO TAIFA

LIGI Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea leo kwa nyasi za viwanja vinne kuwaka moto kwa michezo mikali na ya kusisimua. Mchezo ambao unatarajiwa kuteka hisia za wengi ni kati ya wenyeji Simba SC dhidi ya Prisons ya Mbeya Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mechi nyingine leo ni kati ya Mbeya City na Ruvu Shootings Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, Stand United na Kagera Sugar Uwanja wa Kambarage Shinyanga na Mgambo JKT dhidi ya Coastal Union Uwanja wa Mkwakwani, Tanga. Ikitoka kupoteza mchezo wake uliopita ugenini dhidi ya Stand United, Simba SC leo itajaribu kutuliza hasira za mashabiki kwa kusaka ushindi wa nyumbani. Hata hivyo, hiyo haitakuwa kazi nyepesi kwa sababu Prisons ni timu imara ambayo pia inakabiliwa na shinikizo la kushuka daraja, hivyo katika hatua hii ya lala salama ya Ligi Kuu inatafuta pointi za kuwanusuru kuteremka. Stand na Kagera ni mchezo mwingine unaotarajiwa kuwa mkali hii leo Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga, ambao ni wa nyumbani kwa timu hizo zote. Stand Utd Shinyanga ndiyo nyumbani, wakati Kagera imeamua kutumia Uwanja wa Kambarage baada ya Uwanja wa Kaitaba Bukoba kuingia kwenye ukarabati. Mgambo na Coastal pia Uwanja wa Mkwakwani ni patashika nyingine. Coastal itacheza mechi ya kwanza baada ya kuongeza nguvu katika benchi lake la Ufundi kwa kumchukua kwa muda kocha wa mabingwa wa Ligi Daraja la Kwanza, Mwadui ya Shinyanga, Jamhuri Mussa Kihwelo. Mbeya City nao baada ya kutandikwa mabao 3-1 na Yanga SC katika mchezo uliopita nyumbani, leo watajaribu kurejesha heshima Uwanja wa Sokoine. Vinara wa Ligi Kuu, Yanga SC na mabingwa watetezi, Azam FC wikiendi hii hawapo kwa sababu wamekwenda kwenye mechi za michuano ya Afrika. Yanga SC inayoongoza Ligi Kuu kwa pointi zake 31 za mechi 15, jana ilifungwa mabao 2-1 na wenyeji BDF XI katika mchezo wa marudiano Raundi ya Awali Kombe la Shirikisho nchni Bitswana, kakini imesonga mbele kwa ushindi wa jumk la wa 3-2 baada ya awali kushinda 2-0 Dar es Salaam. Azam FC yenye pointi 27 za mechi 15 pia, leo inashuka dimbani Uwanja wa Merreikh kumenyana na wenyeji El Merreikh katika mchezo wa marudiano Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa Afrika. Azam FC pia ilishinda 2-0 mchezo wa kwanza Dar es Salaam.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: