Magoli mawili yaliyofungwa katika vipindi tofauti na wachezaji Santi Cazorla kwa njia ya penati kwenye dakika ya 24 na mchezaji ambaye yupo kwenye fomu ya hali ya juu kwa sasa Olivier Giroud kwenye dakika ya 66 yameifanya Arsenal kupanda juu mpaka nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi kuu nchini Uingereza.
Licha ya Arsenal kuonekana ni dhaifu kabla ya mchezo huo ilianza kwa kasi mchezo huo na kuifanya safu ya ulinzi ya Manchester City ikiongozwa na Vincent Kompany kufanya makosa.
Ushindi huo wa Arsenal wa magoli 2-0 kwenye uwanja wa nyumbani ya Manchester City Etihad stadium umepunguza kasi kwa mabingwa hao watetezi na hivyo Chelsea kuendelea uongozi wa ligi kuu nchini Uingereza.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment