Mzungu wa Simba apeperusha Sherehe za Ubingwa wa Mapinduzi

Ndoto za Mashabiki na wapenzi wa klabu ya Simba ya Jijini Dares salaam kusherekea ubingwa wa kombe la Mapinduzi ambao timu yao iliunyakua Januari 13 Zanzibar, zimeyeyuka baada ya Kocha Mkuu, Goran Kopunovic, kusema huu sio muda wa kusherekea bali ni muda wa kazi.
Kopunovic amesema kuwa, walijua wakitoka Mtwara watafanya sherehe, lakini baada ya kuifunga Ndanda ugenini sasa anaitengeneza timu kwa ajili ya mechi nyingine.
“Kama unaulizia sherehe haitakuwepo, watu kadhaa wameniuliza kuhusiana na hilo lakini hakuna sababu ya kufanya hivyo. Kuifunga Ndanda hakikuwa kitu lahisi, Walijua baada ya kutoka Mtwara tutafanya sherehe hiyo imeishapita, tumeshinda na sasa tunatengeneza timu kwa ajili ya mechi nyingine” Amesema Kopunovic raia wa Serbia.
Kabla ya Simba kuichapa Ndanda kwa jumla ya mabao 2-0 katika uwanja wa Nangwanda Sijaona, walikuwa wametoka kunyakua ubingwa wa kombe la Mapinduzi huko visiwani Zanzibar, baada ya kuifunga Mtibwar Sugar, kwa mikwaju ya penati 4-3 na kukabidhiwa kombe hilo ambalo lilikuwa kwa KCCA ya Uganda.
Simba walipo tua Dar es salaam januari 14 wakitokea Zenji hawakukaa, ilibidi waunganishe moja kwa moja hadi Mtwara ambako walikuwa wanasubiliwa na Ndanda FC kwa mchezo huo wa ligi kuu Tanzania bara
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: