Wabunge wawili kutoka mkoani Arusha wanatarajia kuanzisha upya mjadala wa kutaka kufukuzwa Bungeni na Spika Anne Makinda iwapo Prof. Muhongo hatakuwa amewajibishwa au kujiuzulu mwenyewe kufuatia maazimio ya Bunge yaliyotaka Waziri huyo wa Nishati na Madini awajibishwe kutokana na kutowajibika katika sakata la Akaunti ya Tegeta Escrow mwaka jana.
Wabunge hao ni Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema pamoja na Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari.
Akizungumzia na wananchi kwenye mkutano wa hadhara jana Manispaa ya Moshi Lema alisema kuwa atakuwa mbunge wa kwanza kufukuzwa katika kikao cha Bunge kijacho endapo Prof. Muhongo atakuwa hajawajibishwa.
Naye Joshua Nassari amesema kuwa atamuunga mkono kutaka maazimio ya Bunge yatimizwe na mamlaka zinazohusika.
Kikao cha Bunge cha 16 na 17 kiliazimia kwamba wahusika wote katika sakata la Akaunti ya Tegeta Esccrow wawajibishwe suala ambalo halijatimizwa na mamlaka zinazohusika kwa upande wa Serikali.
Kwa upande wa waliowajibishwa ni Waziri wa Nyumba na maendeleo ya Makazi Prof .Anna Tibaijuka, Mwanasheria mkuu wa serikali alijiuzulu na kubakia Waziri wa Nishati na Madini Prof Tibaijuka.
Viongozi wengine wa serikali ni wenyeviti wa kamati tatu za Bunge ambao ni Victor Mwambalaswa, William Ngeleja pamoja na Andrew Chenge.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment