Norway yapania kuboresha Sekta ya Afya Nchini Tanzania

Serikali ya Norway tayari imetoa mamilioni ya krone fedha ya nchi hiyo kwa ajili ya kutekeleza Mradi wa kuinua Hospitali ya Kilutheri Hydom msaada ambao Askofu wa KKKT Dayosisi ya Mbulu Mkoani Manyara Nicolaus Nsangazelu ameeleza kuwa umesaidia kupunguza gharama za huduma kwa wakazi wengi wa wilaya hiyo na maeneo ya jirani.
Azma ya Serikali ya Norway kuendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania kuboresha huduma za afya hususani kwa wananchi wa vijijini wanaoishi pembezoni ili waweze kupata huduma zenye uwiano sawa na wanazopata wananchi wengine inatarajiwa kuleta mabadiliko makubwa ya kiafya hasa katika huduma za kimahabara.
Akizungumza katika maadhimisho ya miaka sitini tangu kuanzishwa kwa hospitali ya Hyodom wilayani Mbulu Balozi wa Norway nchini Tanzania Hanne Marie Kaarstad amesema ili kuendelea kuboresha huduma za hospitali hiyo inayoendeshwa na kanisa la kiinjili la kilutheri nchini serikali yake inakusudia kuijengea uwezo wa kufanya utafiti wa kimaabara katika kubaini magonjwa mbalimbali.
Kwa upande wake waziri wa Uwezeshaji na Uwekezaji Dokta Mary Nagu amesema serikali inatambua umuhimu wa afya za wananchi wake kwa muskabali wa maendeleo yao na ya taifa hivyo itaendelea kushirikiana na wadau wa maendeleo kufikia lengo la kuwa na taifa la watu wenye afya.
Maadhimisho hayo ya miaka sitini yametumika kuendesha harambee inayolenga kukusanya fedha kwa ajili ya kuwahudumia wagonjwa wanaoshindwa kumudu gharama za matibabu katika hospitali hiyo ya rufaa ngazi ya mkoa.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: