ONE DAY YES sehemu ya 7

Jivunie kuwa mwana ludewa

ONE DAY YES

Sehemu Ya 7

Mtunzi..... MoonBoy

Simu No. +255714419487 WhatsApp

Ilipoishia Jana ↓

Haaaaa sasa kuangalia chini ya siti nilishangaa kuona miguu ya abiria wote ikitetemeka kwa staili moja.. yaani jinsi inavyotetemeka hawapishani kabisa utafikiri ni madansa wa diamond

Sasa nikajua hapa siii mahari pa kukaa tena. hivyo nilijitahidi kuamka na kutaka kutokea dirishani... Nilivutwa miguu na kupigwa kibao kimoja tu cha utosi.... Kilichonifanya nipoteze fahamu pale pale ndani ya gari

ENDELEAAA



Kutoka hapo sikujua kilichoendelea zaidi... maana sikua najielewa tena.

Nilipokuja kuzinduka nilijikuta nipo ospitalini tena nikiwa nimezungushiwa mabendeji ya kutosha katika mkono na mguu wake wa kushoto. Nilishindwa kujua hapa nilifikaje kutoka katika mikono ya wale watu waliokua wakicheka cheka hovyo,
Ghafla alikuja nesi aliokua akiniuguza hapo odini...
"ooo umeamka mgonjwa?"
"ndio..Eti nani kanileta hapa?"
"aaahh aliekuleta huku ni dokta mkuu"
"ah ah sisemei alionileta humu odini bali nauliza alionileta hospitali"
"mmhh kiukweli sijui labda nimuite dokta?"
"hebu muite"

Basi nesi huyo alitoka hapo na kwenda kumuita huyo dokta wao.... nilikaa kama dakika tano hivi nikisubiria dokta aletwe.. mara dokta kafika wodi hiii
"shkamoo?"
Nilimsalimia dokta huyo mana ni mwanamke wa makamo kiasi.
"marahaba hujambo kijana?"
"sijambo"
"wajionaje hali yako?"
"aaa sio mbaya japo nina maumivu kwa mbali"
"pole sana kijana"
"asante... Aahh eti dokta naomba kujua ni nani kanileta hospitali?"
"mnhh kiukweli hata mimi simjui kwani mtu huyo alioniachia wewe na kulipa matibabu yote lakini sikufanikiwa kuiona sura yake wala kusikia sauti yake.. kwani nakumbuka nilikua natoka lanchi.. lakini ghafla nilihisi mtu ndani ya gari yangu. na ni kweli alikua ni yeye huyo mtu na alikua kakupakata mapajani mwake kama mtoto mdogo"
"ebu ngoja kwanza unasema alinipakata mapajani mwake?"
"ndio alikupakata ukiwa hujitambui"
"mungu wangu eee usikute kanipakata kweli kweli aisee ni jinsia gani uyo mtu?"
"kiukweli mimi sifahamu kwani hakuongea kabisa na alijifunika nguo nyeusi usoni"
"kwa wewe ulivyomuona maumbile yake ni kama dume au jike?"
"jamani kijana huyo mtu alikua kaka nyuma ya siti ya gari yangu hivyo kutokana na alivyonionya. ikanibidi nikubali kisha akatoweka hapo hapo kwenye gari"
"mungu wangu eee kama ni kidume basi kitakua kimenipakata kweli dokta daahh"
"lakini yule mtu nadhani sii binadamu wa kawaida kwakweli"
"mmhh ok sawa"
"lakini kwani ulikua unaelekea wapi?"
"nilikua naelekea arusha kwani hii ni hospitali gani?"
"hii ni hospitali ya mount meru arusha"
"mmhh haya sawa ila nina muda gani ndio nitoke?"
"lazima ukae kama mwezi hivi"
"mwezi? ayaaaa nwezi wa nini dokta?"
"ndio ni kutokana na hali ulionayo"
"aaa fanya wiki tu dokta"
"tutaangalia kama utakua vizuri"

Basi niliendelea kukaa pale hospitalini huku nikiuguza mguu wa kushoto na mkono wa kusho.. nilikua nimening'inizwa juu. huku limfuko lizito likinielemea ili mfupa uungane katika hali yake ya kawaida

BAADA YA SIKU 6 KUPITA

bado nilikua nipo hospitalini na matibabu yalienda vizuri kabisa Hivyo sikua na wasi wasi juu ya chochote kile. Dokta yule alikuja na kunipa pole huku akionekana kunizoea kwa ucheshi wangu wa hapa na pale. Nesi ilibidi aniulize kitu
"eti kijana?"
"ndio dokta?"
"mbona toka umeletwa sasa yapata wiki lakini hakuna ndugu wala jamaa aliokuja kukuona"
"aaahh kiukweli dokta mimi hapa sina mtu ninayemjua hapa mjini. ila nilikua naenda kwa kaka yangu aliopo huku mjini ila pia sijui anaishi wapi"
"oo pole sana kwani huna namba zake za simu?"
"kiukweli sina dokta"
"haaaaa yani kaka yako ukose kua na namba zake?"
"ni stori ndefu dokta"
"mmhhh haya mana nimekuuliza hivyo kwasababu bili uliolipiwa sasa imekwisha.."
"ooo shit sasa itakuaje dokta?"
"mnhh kiukweli mimi sijui cha kufanya tena"
"au niruusu tu nikamtafute kaka yangu"
"hapana haitokua sawa kukuruhusu kwani hapo ulipo bado mifupa haijaunga"
"hivyo hivyo dokta itaungia mbele ya safari huko kwa kaka angu"
"sasa si ulisema humjui anapoishi wewe?"
"ndio sijui anapoishi lakini kutokana na umaarufu wake huenda nikamjua kwa bahati tuu"
"kwani kaka yako anafanya kazi gani?"
"mnhh niliskia ni mtu wa madini sjui nani vilee sijui boko baku aaa mi sijui bwana"
"Au ni broka"
"Eenheee hivyo hivyo eee"
"anaitwa nani?"
"anaitwa hatibu"
"hatibu? hatibu huyu huyu tajiri mkubwa wa hapa arusha nzima?"
"mnhh mi sijui kama ana utajiri huo.. ila ni mrefu afu mweusii ana mimacho mikubwaaa"
"Basi atakua ndio huyo. mana hata huyu tunaemjua ni hivyo hivyo"
"basi ndio huyo aisee naomba niruusu tu"
"basi nitakupeleka jioni sawa?"
"sawa"

Ilipofika mida ya jioni dokta alinichukua huku nikiwa na magongo yangu kwa ajili ya kupelekwa kwa broo wangu mkubwa. Simu yangu nilikua nayo ila nguo tu ndio sina maana vilipotea katika ile ajali iliotokea pale... Dokta huyu alinifikisha hadi huko anapoishi kaka yangu... maana ni maarufu sana hivyo hakuna mtu asiejua nyumbani kwake,

Dokta aliniacha na kuondoka zake nami nilimshukuru sana kwa msaada wake...
Basi niligeuka na kuanza kubonyeza kitufe cha kengele ili nifunguliwe mlango. Kiukweli kaka angu alikua ana mjumba mkubwa tena ni wa gholifa kabisa.
sasa Mlinzi alikuja na kuniuliza
"samaani nikuseidie nini?"
"aaa samahani kaka mimi ni ndugu yake na hatibu"
"Eti nini? yani wewe kapuku uwe na ndugu kama huyu?"
"Aahh sheheee hatibu ni kaka yangu"
"hebu ngoja nimuite mkewe kwanza"
Nilisubiri hapo nje ili mke wa broo aje aniambie ni kweli... lakini kibaya zaidi hata huyo mke mwenyewe hanijui wala simjui. maana kaka ana muda mrefu toka aje mjini hajawahi kurudi kijijini hata siku moja, kwahio hata kuoa kwake sisi hatujui kabisaa

Mara mke wa kaka akaja huku akisema kwa dharau nyingi mno
"yuko wapi huyo kapurwa unaemsemea wewe?"
"si huyu hapa nje na miguu yake iliovunyika utafikiri kadondikewa na meli"
"heeeeeeee we vipi umepotea njia?"
Aliniuliza huku akiniangalia chini juu Nilikua naona aibu kwa dharau ninazofanyiwa afu ukiangalia ni mtu na familia yangu..
"mimi ni ndugu yake na broo"
"heeee ivi ana akili timamu huyu?"
"sijui hebu muulize"
"we mbaba eti una akili vizuri wewe?"
"ndio na namfahamu kaka angu na yeye pia ananifahamu"
"sisi tutakuaminije wewe? Ok kwa kifupi we kaa hapo nje umsubiri mpaka aje akuone ndio uingie nae ndani sawa?"
"mmhh sawa"

Walifunga geti lao kwa hasira huku wakiongea maneno machafu ambayo sikuyapenda kwakweli.
Sasa mida hio kumbuka ni mida ya jioni na kagiza kalikua kakiingia Afu broo ndio bado hajaja na nikiangalia juu mvua ilikua ikija kwa upepo mkali
Nilikua sina hata sehemu ya kujificha ili mvua ipite... hivyo ilininyeeshea pale pale nje ya geti huku yale mabendeji niliofungwa yakaanza kulegea na kunipa maumivu makali kweli... Nilivumilia hadi ilipofika mida ya saa tatu.. ndio nikaona mwanga wa gari ukija na huku getini.. Na alikua ni yeye ndio anarudi kutoka kazini. sasa alipofika pale alishuka na kuja kuniuliza maswali ya ajabu ajabu tu..
"we ni nani wewe?"
"broo ina maana umenisahau?"
"mi sina ndugu mjini bwana we sema we ni nani?"
"ni mimi rashidi bakari kingazi"
"ni nani kakuelekeza hapa?"
"nimeulizia tuuu"
Nilikua naongea kiunyonge sana ili asije akanikataa tu maana sina pakulala kabisa
"mmhh umetumwa?"
"wala tu broo nimekuja kutafuta maisha"
"lakini kwanini usinipe taarifa kama unakuja?"
"lakini broo namba zako tungetoa wapi?"
"mschiiiiuuuuuu ( msunyo ) haya ingia ndani"
Daa nilishukuru kwa kuskia hivyo kwani hata vile alivyosema sina ndugu mjini alikua ananitishia tu... Basi alipiga honi na geti likafunguliwa na kuingia yeye na mimi pia...

Tulipofika ndani mke wake akaja juu
"heee ivi kweli ni lindugu lako hili?"
"aaaa si unajua mambo ya vijijini ndio ni ndugu yangu"
"mmhhh mbona hata hufanani nae kabisa huyu?"
"mmhhh we muache tu"

Tuliingia mpaka ndani sebuleni na kukaa kwenye sofa kalii lakini nilikalishwa chini na shemeji eti ninachafua sofa
"vp mbona umefungwa fungwa miguu mikino nini shida?"
"aaahhh nilipokua nakuja tulipata ajali hivyo nilipelekwa hospitalini?"
"mmhhh haya bwana vp una njaa?"
"ndio broo"
Akaitwa mfanyakazi na kuambiwa akaniletee chakula... Daa tena siku hio walipika hubwa hubwa kitu cha kipunga... Daahh nilikifakamia kama mbwa yani...
"kwaio una kama wiki toka uje arusha?"
"ndio broo"
"pole"
"mmhh asante ila broo wazazi wanakuulizia sana broo"
"habari za nyumbani sizitaki kabisa kuzisikia... na kama umeletwa na njaa njaa zako na shida zako utarudi ulipotoka"
"basi broo yaishe"

"mama omari?"
"abee?"
"hebu toa yale masuruali na mashati yalioniruka mpe abadili hizo nguo"
Nilishangaa kuskia hivyo
"haaaaaa"
"haaa nini?"
"sasa mwili wako broo na mimi kweli si itakua kama gunia?"
"kama hutaki acha"
"ah ah ok ntazivaa tu"
Baada ya hapo nilipelekwa stoo ambako kunawekwa mikaa na vyuma vyuma na pia kuna sehemu ya lile dude la kufulia nguo. afu kwa pembeni kuna kitanda.. ambacho mtu akija kufua nguo zake kama zinachelewa kidogo basi anajilaza hapo... sasa hicho ndio kitanda changu...

Nilipewa na shuka moja tu la kujifunika.... ila mi sikua najali kitu kikubwa mambo yangu yaende sawa tu.... Nilibadili zile nguo mbichi na kuvaa suruali hio kubwaaa kama suruali ya MADILUU unamjua madiluu wewe? sasa ndio hiii bwana.
Niliivaa na kuifunga na kamba ya mkonge. Nili lala vizuri tu wala sikua na shaka na mtu... maana nishazoea maisha ya shida sana tuu
hivyo haya naona ni ya kawaida tu kwani hata broo anaonekana hakupendezewa na ujio wangu kabisa.....

Sasa nikiwa nimelala zangu mara mlango uligongwa..
Nikajikongoja na kwenda kufungua.. Alikua ni mfanya kazi wa kike amekuja kuchukua mkaa... maana huko niliko si stoo ya vitu...
"mambo?"
"poa"
"sijui unaitwa nani?"
"naitwa rashidi"
"ok na mimi naitwa hadija"
"oohh nashukuru kukufahamu"
"mnhh huyu baba ni ndugu yako kabisa?"
"ndio ni ndugu yangu kabisaa"
"sasa mbona kakulaza huku?"
"mhhh mi sijui mipangilio ya nyumba yao"
"mhhh ila kaka hii nyumba sijui kama utaweza kuishi kweli"
"kwanini useme hivyo?"
"hii nyumba tatizo lake ni"
Mara aliitwa na shemeji
"we hadija?"
"abee?"
"unafanya nini huko?"
"nachukua mkaa"
"hebu fanya haraka"
"sawa dada"
Basi mtoto akawa anaendelea kusema Lakini kabla hajaendelea na stori niliona mtu kakaa juu ya ile mashine ya kufulia nguo afu kavaa nguo nyeupeee afu ni chafu...
Ikabidi nimuulize huyu hadija ili nisije kukiwazia vibaya bure
"Eti we hadija?"
"nini?"
"unamjua yule jamaa pale?"
"jamaa gani wewe huku hakukaagi watu"
"jamani mtu si yule pale anatuangalia"
"yesu wangu kimbia wewe"

Sasa mfanyakazi alitupa ndoo ya mkaa na kukimbia... nami nikajaribu lakini nilishindwa kukimbia kwasababu ya mguu wangu na mkono hivyo nilibaki nikijiburuza tu chini kama paka aliokatwa kiuno... Sasa nikiwa najiburuza mara yule jamaa akatokea tena kwa mbele... Lakini nilipoiangalia hio sura ni kama naifahamu vile....
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: