VETA WASAJILI VYUO 19 MKOA WA NJOMBE.
Mamlaka ya mafunzo ya ufundi stadi VETA kanda ya nyanda za juu imetoa vyeti kwa vyuo 19 vya mkoa wa Njombe baada ya kupata usajili wa awali ambao utadumu kwa miaka miwili na kuwataka wamiliki wa vyuo hivyo kufundisha fani walizosajiliwa sambamba na kuhakikisha wanaongeza fani za masomo katika vyuo vyao.
Akiongea katika makabidhiano ya vyeti hivyo kaimu mkurugenzi wa VETA nyanda za juu kusini Bi Susan Magani amesema kuwa kila mmiliki wa chuo anatakiwa kutoridhika na idadi ya fani anazotoa kwani ananafasi ya kusajili nyingine ili kuendana na mahitaji katika jamii kwa wakati husika
Naye mratibu wa mafunzo kanda nyada za juu John Mwanja amewataka wamiliki wa vyuo hivyo kutambua tofauti ya madaraja, na kuacha tabia ya kufaulisha wanafunzi kwenye vyuo vilivyosajiliwa sambamba na kuhakikisha wanakuwa mabalozi wa kutoa taarifa ya kutokuwepo kwa vyuo visivyosajiliwa huku akieleza kuwa usajili huo ni hatua ya kuanza kupambana na vyuo feki katika kanda.
Amevitaja vyuo vilivyosajiliwa na kupewa vyeti katika mkoa wa Njombe kuwa ni pamoja na chuo cha matembwe vts ,the profesional college of njombe, chuo cha lukungu vtc na kipengele vtc igwachanya vtc
Kwa upande wao wamiliki na wakuu wa vyuo wameitaka Mamlaka hiyo kuhakikisha inaonyesha meno yake kwa kuvifungia vyuo visivyo na usajili ili kuwarahisishia wanafunzi kutokupata elimu isiyostahiki, na kukiri kuwa usajili huo walioupata utawapa chachu katika ufundishaji kwa mitihani itatungwa na mamlaka ya mafunzo na ufundi stadi VETA
Uongozi huo wa mamlaka ya VETA kanda ya nyanda za juu umesema kuwa usajili huo ni wa kwanza kwa mkoa wa Njombe tangu kufutwa kwa usajili wa vyuo vyote nchini kutokana na kuwepo kwa vyuo ambavyo havina sifa hivyo kuanza kusajili upya.
Jivunie kuwa mwana ludewa
Blogger Comment
Facebook Comment