WANAUME WILAYANI LUDEWA WATAHIRIWA KUEPUKA UKIMWI

SERIKALI wilayani Ludewa inaendelea kuwafanyia tohara wanaume wasiotahiriwa ikiwa ni moja ya mikakati yake ya kuzuia kuongezeka kwa maambukizi mapya ya Ukimwi kwa wakazi wake.
Hatua hiyo imetokana na wataalamu kubaini kuwa, kuna uhusiano mkubwa kwa wanaume wasiotahiriwa na ongezeko la maambukizi mapya ya Ukimwi.
Takwimu za kitaifa zinaonesha kuwa wilaya hiyo ina asilimia 6.1 ya maambukizi na Mkoa wa Njombe ndiyo unaoongoza kitaifa kwa kuwa na wastani wa asilimia 7.
Mkuu wa Wilaya hiyo, Juma Madaha, alisema hayo mwishoni mwa wiki wakati akizungumza ofisini kwake kuhusu mkakati wa kupambana na maambukizi mapya ya ugonjwa huo ambapo kwa sasa umepata mafanikio makubwa.
Kwa mujibu wa Madaha, Wilaya ya Ludewa ni miongoni mwa maeneo ambayo yameathirika kwa kiasi kikubwa kwa Ukimwi na kunatakiwa juhudi kubwa na za makusudi kupunguza tatizo hilo ikiwamo kuongeza elimu ya uelewa wa athari kwa wananchi.
Alieleza kuwa, hapo mwanzo mapambano dhidi ya Ukimwi yalikuwa magumu na tatizo kubwa lilionekana kuwepo kwa idadi kubwa ya wanaume wasiotahiriwa hivyo kwa namna moja na nyingine kuchangia kuongezeka kwa tatizo.
Madaha alisema, pamoja na hatari ya kupata Ukimwi kwa urahisi, lakini pia kutofanyiwa tohara kwa wanaume kunasababisha maambukizi ya ugonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi kwa wanawake jambo ambalo ni hatari kwa afya na kusababisha vifo.
Aliwataka wakazi wa wilaya hiyo kuwa waangalifu na nyendo zao na kujiepusha na tabia inayoweza kuwasababishia kupata maambukizi mapya kwa kuepuka kufanya ngono zembe.

Jivunie kuwa mwana ludewa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment