Mchungaji afa na miaka 114, mjane ana miaka 30

MCHUNGAJI Samuel Sadela (114), wa Kanisa la Gospel Apostolic huko Nigeria aliyehubiri kwa miaka 82 amefariki dunia na kuacha mjane mwenye umri wa miaka 30 aitwaye Christina aliyemuoa miaka saba iliyopita.
Mchungaji Sadela alioa mke wa tatu, Christina mwaka 2007, baada ya kufiwa na mke wake wa pili mwaka 1965 ambaye alizaa naye watoto wanne na wawili kati ya hao walifariki na mkewe huyo alifariki mwaka 2001.
Awali, Ofisa Mwandamizi mmoja wa juu wa kanisa hilo lililopo kwenye Wilaya ya Gdagada, Lagos aliviambia vyombo vya habari vya kimataifa kuwa, mchungaji huyo alifariki dunia Jumapili iliyopita baada ya kuugua kidogo maradhi yanayohusishwa na uzee kutokana na umri wake.
“Papa (Sedela), amekufa baada ya kuugua muda mfupi, tunamkumbuka mchungaji wetu na mlezi wa kanisa enzi za utumishi wake,” alisema Ofisa huyo ambaye hakutaka jina lake litajwe.
Mchungaji Sadela, alisifika sana kwa huduma yake na kusafiri maeneo mengi ndani na nje ya Nigeria akihubiri neno la Mungu na nchi alizowahi kuhubiri ni kama vile Marekani na Uingereza na kwamba alikuwa akisisitiza kuwa amezaliwa mwezi Agosti, mwaka 1900, ingawa hakuna nyaraka zinazothibitisha hilo.
Taarifa zinasema, ikiwa ni kweli mchungaji huyo amezaliwa mwaka huo, basi angekuwa ndiye mtu mwenye umri mkubwa zaidi duniani kwa mujibu wa Kitabu cha Maajabu ya Rekodi za Dunia.
Mamia ya waombolezaji wa kanisa hilo walionesha huzuni zao huku wakijipanga kwenye mstari mrefu kwenda kusaini kitabu cha maombolezo kilichowekwa kwenye viwanja vya kanisa hilo.
Kabla ya kuoa mke wake wa pili, Papa Sedela alikuwa na mke wa kwanza ambaye alizaa naye watoto saba, ambao pia wote walifariki wakiwa wadogo na mkewe huyo akafa baada ya miaka 21 ya ndoa.
Katika enzi za uhai wake alikuwa akisema anajisikia kijana na mwaka jana alisherehekea siku ya kuzaliwa kwake akiadhimisha miaka 113 na kusema anaamini Mungu atamuweka aishi miaka mingi zaidi

Jivunie kuwa mwana ludewa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment