ninakuhabarisha kutoka ludewa njombe tanzania
NJOMBE
Katibu
Mkuu wa Chma cha mapinduzi,CCM, Abdulrahman Kinana, amesema chama
hicho kinawajibu wa kuisimamia serikali, katika kuhakikisha
inapunguza urasimu na kuandaa mazingira mazuri, yatakayowawezesha
vijana kujiajiri ili kuondokana na tatizo la ajira nchini.
Kinana
aliyasema hayo, katika kijiji cha Isuka, wakati akizungumza na vijana
100, walioanzisha kituo cha mafunzo ya zana za kilimo, kwa wakulima
wilayani Wanging'ombe mkoani Njombe, kwa lengo la kijishughulisha na
kilimo cha mazao mbalimbali.
Alisema
vijana wana nafasi kubwa ya kutumia fursa za kilimo ili kuendeleza
maisha yao na baadaye kujiajiri badala ya kusubiria ajira na matokeo
yake kujikuta wakiishi kwa matumaini bila ya kujua maisha yao
yatakuwaje.
Alisema
kuwa vijana wanatakiwa kukaa chini kufikiri na kuamua na kazi ya
serikali itakuwa kutimiza mipango yao kwa kuwaandalia mazingira ya
kujiajiri na kupata fursa za mikopo itakayowawezesha kuanzisha miradi
ya maendeleo.
Wakati
huo huo Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Dar es Salaam, leo
kimeandaa mapokezi makubwa ya Katibu Mkuu wao, Abralrahaman Kinana ,
kufuatia kumaliza ziara katika mikoa ya Ruvuma, Mbeya na Njombe.
0 comments:
Post a Comment