ninakuhabarisha kutoka ludewa njombe tanzania
Na barnabas njenjema,Ludewa

mbunge wa jimbo la ludewa akiongea na waitimu

picha ya pamoja na wahitimu wa mafunzo pamoja na mh. deo filikunjombe
Na barnabas njenjema,Ludewa

mbunge wa jimbo la ludewa akiongea na waitimu
picha ya pamoja na wahitimu wa mafunzo pamoja na mh. deo filikunjombe
Mbunge
wa jimbo la Ludewa Mh.Deo Filikunjombe amewahakikishia wananchi wake
kuwa na matumaini ya ujenzi wa chuo cha VETA, katika kijiji cha
shaurimoyo kata ya Lugarawa, pamoja na kuwaomba madereva kuwa makini
wawapo barabarani.
Akizungumza
katika mikutano ya hadhara, katika kata za lugalawa,mlangali , milo
pamoja na ludewa, katika sherehe za kuitimisha mafunzo ya udereva
wa muda mfupi, kutoka chuo cha veta songea, kwa kushirikiana na ofisi
ya mbunge wa jimbo la ludewa pamoja na kugawa vyeti pamoja na leseni katika sherehe hizo.
Chuo cha veta tawi la songea kinajihusisha na utoaji wa mafunzo kwa lika zote kwa kozi mbalimbali kama vile edereva wa muda mfupi na muda mrefu,ufundi wa magari ,ufundi wa nyumba ,ufundi wa umeme,ushonaji,utengenezaji wa sabuni pamoja na batiki
Filikunjombe
amesema, Serikali imeamua kuanza ujenzi huo kutokana na umuhimu wa
wananchi wa ludewa, ili kupata fursa ya kujifunza mafunzo mbalimbali
kutoka chuo cha VETA
Pia amewasisitiza wahitimu wa mafunzo hayo kutoka chuo cha veta songea kuwa makini wawapo barabarani kwani anawategemea katika shughuli mbalimblia hasa katika msimu huu wa kuelea uchaguzi mkuu
Naye
mkurugenzi wa VETA kanda ya mikoa ya kusini Bi.Monika Mbele,
amewahakikishia wananchi wilayani wa wilaya ya ludewa kwa uvumilivu wao tangu walipotangaziwa kuanza kwa ujenzi wa chuo cha veta katika kata ya lugarawa,
ujenzi huo unatarajiwa utaanza ujenzi hivi
karibuni, na hatua mbalimbali za ujenzi zimeshaanza ikiwa ni pamoja
na ramani ya majengo na kuweka mipaka ya chuo ambapo kitajengwa.
kwa upande wa kamanda wa kikosi cha barabarani Mkoa wa Njombe Maro Chacha amewasisitiza wahitimu hao kufuata sheria za na alama za barabarani ili kupunguza ajari za makusudi wazipatazo madereva wa bodaboda,
pia ameongeza kuwa ni muhimu kwa kila dereva kutambua abiria wao kama wanania nzuri au mbaya hasa nyakati za usiku kuepukana na ajari mbalimbali za kuibiwa vyombo vyao vya usafili na wakati mwingine kuuwawa .
Kwa
upande wao wanafunzi waliohitimu mafunzo hayo katika kata za Lugarawa,Mlangali,Milo pamoja na ludewa wamemshukuru
Mh.filikunjombe kwa jitihada zake za kuwaletea maendeleo wananchi wa
LUDEWA na jitihada zake za kujituma katika kuhakikisha anatumia vizuri nafasi aliyopewa na wananchi wa jimbo la Ludewa .
katika hatua nyingine Mh.Mbunge wa jimbo la Ludewa M.Deo filikunjombe amewaomba chuo cha VETA kuendelea kutoa mafunzo Wilayani hapa kwa kozi mbalimbali hadi hapo chuo cha VETA cha Ludewa kitakapokamilika
0 comments:
Post a Comment